IQNA

Nakala ya kihistoria ya Qur'ani imehifadhiwa kaskazini mashariki mwa Cairo

16:45 - August 05, 2024
Habari ID: 3479231
IQNA – Nakala adimu na ya kale ya Qur'ani Tukufu, iliyoandikwa karne nne zilizopita, imehifadhiwa katika kijiji kaskazini mashariki mwa Cairo, Misri.

Nakala hii, ya mwaka 1028 AH (1618 Miladia), inahifadhiwa na watu katika kijiji cha Birkat al-Hajj.

Nakala hii ya Qur'ani Tukufu, pia inajulikana kama Mushaf Matbouli, kwa sasa inalindwa na familia ya Mahmoud Abdul Ghaffar, mkazi wa kijiji hicho. Wakati wa ukarabati wa Msikiti wa Matbouli, Abdul Ghaffar aliipeleka Quran nyumbani kwake kwa ajili ya ulinzi, Arabi 21 iliripoti.

Nakala hiyo ina urefu wa sentimeta 40 na upana wa sentimita 28, uzani wa zaidi ya kilo 5.75.  Nakala hii haijumuishi maandishi ya Qur'ani tu bali pia tafsiri na maana za maneno pembezoni.

Abdul Ghaffar alitaja kwamba mashirika mengi, ikiwa ni pamoja na Wizara ya Wakfu ya Misri, yamejaribu kupata hii Qur'ani. Hata hivyo, wanakijiji wamekataa kwa uthabiti, na kuhakikisha kuwa muswada huo unabaki chini ya uangalizi wao, kama walivyokabidhiwa na imamu wa msikiti huo.

Saber al-Qazi, mtaalamu wa kazi za kihistoria, amesema kwamba hati hii ndiyo nyenzo pekee iliyobaki kutoka karne za mwanzo za Kiislamu katika kijiji hicho.

Kwa karne nyingi, kijiji cha Birkat al-Hajj kimekuwa kituo muhimu kwa Mahujaji kutoka Misri na nchi za Kaskazini na Magharibi mwa Afrika.

Mbali na aya na surah za Qur'ani, Mushaf huu wa kihistoria una Asbab al-Nuzul (sababu au mazingira ya wahyi), uainishaji wa aya kama Makkai au Madani, na ufafanuzi wa wanazuoni mashuhuri.

3489379

Kishikizo: nakala qurani nadra
captcha