IQNA

Mus’haf wa kihistoria wa ‘Kufi’ waonyeshwa katika Makumbusho ya Qur'ani ya Makka.”

9:33 - January 24, 2026
Habari ID: 3481840
IQNA – Nakala ya kihistoria na yenye thamani kubwa ya Qur'ani Tukufu, inayojulikana kama “Qur'ani ya Kufi,” imewekwa wazi kwa umma katika Makumbusho ya Qurani ya Makka.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Iraq, Makumbusho ya Qurani Tukufu mjini Makka limeonyesha moja ya nakala adimu zaidi za Qur'ani, yenye thamani ya juu sana ya kihistoria.

Mus’haf wa Kufi ni nakala inayochukuliwa kuwa ushahidi muhimu katika hatua za awali za ukusanyaji na uandishi wa Qur'ani Tukufu.

Nakala hii ni ushahidi bayana wa maendeleo ya sanaa ya hati za Kiislamu katika karne za mwanzo baada ya kuingia kwa Uislamu.

Nakala hiI ni ya karne ya pili au ya tatu Hijria (karne ya nane au ya tisa Miladia), na imeandikwa kwa hati ya Kufi juu ya ngozi ya mnyama, ambayo inachukuliwa kuwa miongoni mwa vifaa vya kale kabisa vilivyotumika kuandikia Qur'ani.

The Quran Museum in Mecca, Saudi Arabia

Ripoti inaeleza kuwa Mus’haf huu una muundo wa mlalo, mtindo uliokuwa wa kawaida katika hatua za awali za uandishi wa Qur'ani, na unaakisi sifa za kisanaa na kiteknolojia za kipindi hicho cha kihistoria.

Mus’haf huu  unaanza na aya ya 50 ya Surah Al Imran na unaendelea hadi mwisho wa Surah Abasa, na ni mfano wa nakala za sehemu za Qur'ani zilizokuwa maarufu katika nyakati za mwanzo.

Habari inayohusiana:

Aina hii ya nakala za Qur'ani ilitumika kwa madhumuni ya elimu, kuhifadhi Qur'ani na kusambazwa miongoni mwa wanazuoni na wanafunzi wa elimu za dini.

Kuonyeshwa kwa Mus’haf huu kunakwenda sambamba na dhamira ya Jumba la Makumbusho ya Qur'ani Tukufu la Makka ya kutambulisha hazina za Qur'ani na nakala adimu, huku lengo lake likiwa kuwafahamisha wageni kuhusu historia ya Qur'ani Tukufu, mabadiliko ya hati ya Kiarabu, na jitihada za Waislamu katika karne mbalimbali za kuilinda na kuiandika Qur'ani kwa namna iliyo ya kupendeza na yenye heshima ya juu kabisa.

4329829  

Habari zinazohusiana
captcha