IQNA

New York Times: Nguvu za kijeshi za Iran ni zaidi ya alivyotarajia Trump

13:26 - March 16, 2026
Habari ID: 3482061
IQNA-Gazeti moja la Marekani limekiri uwezo wa kijeshi wa Iran wa kuathiri uchumi wa dunia kwa kudhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, gazeti maarufu la Marekani la The New York Times limeripoti kwamba uwezo wa Iran wa kusababisha misukosuko katika uchumi wa kimataifa umevuka matarajio ya serikali ya Trump.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa serikali ya Trump sasa inakiri kwamba uwezo wa Iran wa kuvuruga uchumi wa dunia kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz ni mkubwa zaidi kuliko walivyodhani awali. Eneo hilo ni njia pekee ya baharini inayotumiwa na meli zinazotoka au kuingia Ghuba ya Uajemi. Karibu asilimi 20 ya mafuta yote yanayotumika duniani hupitia njia hiyo.

Gazeti la Marekani la The Wall Street Journal pia hapo awali liliripoti kuwa jeshi la Marekani lilikuwa limemuonya Trump kwamba kulenga Iran kunaweza kuisukuma nchi hiyo kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz. Hata hivyo, Trump aliwaambia wasaidizi wake kwamba Iran ingetangulia kusalimu amri kabla ya kuchukua hatua hiyo.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa Pentagon ina wasiwasi kwamba meli za kivita zinazolinda meli za mafuta katika eneo la Mlango-Bahari wa Hormuz zinaweza kulengwa.

Katika sehemu ya mwisho ya ripoti hiyo inasisitizwa kuwa washauri wa Trump wanamtaka atafute njia ya kujiondoa katika vita vya sasa, lakini bado hana mpango wa wazi wa kuvimaliza. Senario nyingine inayotajwa kwa kumaliza vita ni Trump kutangaza ushindi kisha kujiondoa.

Itakumbukwa kuwa, Marekani na Israel zilianzisha hujuma za kigaidi dhidi ya Iran Jumamosi ya tarehe 28 Februari  sawa na 10 Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kumuua shahidi  Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, makamanda kadhaa wa kijeshi, na mamia raia wakiwemo watoto wadogo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa itaendeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Operesheni ya Ahadi ya Kweli 4, ili kuwaadhibu vikali maadui walioanzisha uchokozi.

4341097

captcha