IQNA

Hatua ya awali ya Mashindano ya Kimataifa la Kuhifadhi Qur’ani ya Misri

16:19 - March 29, 2026
Habari ID: 3482101
IQNA – Mitihani ya hatua ya awali ya Mashindano ya 33 ya Kimataifa la Misri la Kuhifadhi na Kufahamu Qur’ani Tukufu yanatarajiwa kuanza siku ya Jumapili, tarehe 5 Aprili.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Awqaf ya Misri, mitihani hiyo itafanyika katika ofisi za tawala za kikanda kote nchini Misri na itaendelea hadi tarehe 15 Aprili, kama ilivyoripotiwa na gazeti la Misri Al‑Youm.

Baada ya kuthibitishwa kwa sifa za washiriki kulingana na vigezo vilivyotangazwa, wizara hiyo imechapisha majina ya wale waliothibitishwa kushiriki katika mitihani hiyo.

Mitihani itafanyika katika ofisi husika kwa kufuata masharti na vigezo vilivyowekwa.

Wizara imewataka  washiriki kuzingatia maelekezo yanayohusiana na mitihani hiyo na kuhakikisha wanahudhuria kwa nyakati zilizopangwa. Imesisisitiza kuwa kuzingatia kikamilifu vigezo vilivyowekwa kunahakikisha usawa wa fursa na uwazi miongoni mwa washiriki wote.

Mitihani hii itafanyika katika matawi mbalimbali, jambo linaloonyesha tofauti za viwango vya kuhifadhi na kufahamu Qur’ani Tukufu. Tukio hili ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Awqaf za kuhamasisha kuhifadhi Qur’ani, kufahamu maana zake, na kuwatambua wasomaji na wahifadhi wa Qur’ani walio bora na wenye elimu.

 

3496913

captcha