
Siku ya Alhamisi, Kazem Jalali alikutana na Mufti Hazrat Ravil Gaynutdin, Mwenyekiti wa Baraza la Mufti la Shirikisho la Urusi, na kumfikishia ujumbe wa pongezi na shukrani wa Ayatollah Khamenei.
Hatua hii ilifuatia ujumbe wa rambirambi uliotumwa na Baraza hilo kwa Kiongozi wa Mapinduzi, kufuatia kuuawa kishahidi kwa aliyekuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, katika shambulio la kigaidi la Marekani na Israel tarehe 28 Februari.
Katika mkutano huo wa Alhamisi, balozi wa Iran alithamini misimamo ya Mufti Gaynutdin pamoja na tamko la mshikamano lililotolewa na Waislamu wa Russia kuunga mkono wananchi wa Iran katika kukabiliana na hujuma za Marekani na Israel.
“Iran haijawahi kushambulia nchi yoyote, bali Marekani ndiyo iliyoshambulia nchi yetu mara mbili katikati ya mazungumzo, kwa njia ya udanganyifu,” alisema.
Akisisitiza kuwa usalama na uthabiti katika Ghuba ya Uajemi lazima ulindwe na nchi za eneo hilo lenyewe, alikumbusha kuwa miaka iliyopita, kiongozi aliyefariki kishahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliwaalika nchi zote za Ghuba ya Uajemi kusimamia usalama wao wenyewe.
“Nchi za Kiarabu ni ndugu na marafiki zetu. Hatukuwahi kuwa na nia ya kuwashambulia, wala hatujawahi kufanya hivyo. Lakini badala ya kuimarisha usalama wa kikanda, walifanya kosa kubwa kwa kukabidhi jukumu hilo kwa wakandarasi wa Kimarekani,” aliongeza.
Akieleza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yaliirejesha Iran katika safu ya Umma wa Kiislamu, Jalali alisema nchi za Kiarabu zinapaswa kujiuliza ni kosa gani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanya hadi kushambuliwa kutoka katika ardhi yao leo.
Alisema pia kuwa tatizo la utawala wa Kizayuni si Iran pekee, bali haukubali uwepo wa nchi za Kiislamu zenye nguvu katika eneo. “Iwapo, kwa mtazamo wa Magharibi, suala la Iran lingetatuliwa—jambo ambalo halitatokea—basi zamu itakuwa ya nchi nyingine za Kiislamu,” alisema.
“Ili kukabiliana na njama hii, ni lazima turejee mafundisho ya Qur’an Tukufu: umoja na kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu.”
Kwa upande wake, Mufti Gaynutdin alimshukuru Kiongozi wa Mapinduzi na kutangaza upya mshikamano wa Waislamu wa Shirikisho la Russia na serikali pamoja na wananchi wa Iran dhidi ya hujuma za utawala wa Kizayuni na Marekani.
Alisema Waislamu wa Russia wanaunga mkono Iran na kwa dhati wanavutiwa na uthabiti, subira na ujasiri wa taifa la Iran.
“Wavamizi walinuia kuwachochea wananchi dhidi ya serikali kwa kuivamia Iran, lakini taifa la Iran lilibomoa mipango yao mibaya kwa mshikamano na umoja wake, alisema.
Mwenyekiti wa Baraza la Mafti la Shirikisho la Russia pia alirejea njama ya utawala wa Kizayuni na Marekani ya kuzichonganisha nchi za Kiarabu na Iran, na kupandikiza mifarakano ndani ya Umma wa Kiislamu.
Alisema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilizijulisha nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi kwa uwazi na uaminifu, kupitia jumuiya ya kimataifa, kwamba endapo mashambulizi dhidi ya Iran yatafanywa kutoka katika kambi za Marekani zilizo katika nchi hizo, basi Iran italazimika kushambulia kambi hizo.
Alisisitiza kuwa vituo vya kijeshi haviwezi kuhakikisha usalama na utulivu wa kweli, na kwamba nchi za Kiarabu sasa zimeanza kutambua hilo.
“Endapo Waislamu watakuwa na mshikamano na umoja, basi kambi ya kishetani haitaweza kamwe kurudia hujuma zake dhidi ya Gaza, Syria, Iran na Lebanon,” alihitimisha.
4349665