IQNA

Mwanazuoni wa Iran Amwandikia Papa kuhusu uchokozi wa Marekani na Israel

17:38 - March 07, 2026
Habari ID: 3482025
IQNA – Mwanazuoni mmoja wa Iran amemtumia barua kiongozi wa Kanisa Katoliki, akionya kuhusu athari na matokeo ya uchokozi unaoendelea wa Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Iran.

Ayatullah Seyed Mostafa Mohaqqeq Damad, mwanazuoni wa Fiqhi na sheria, katika barua yake kwa Papa Leo XIV alirejelea kuuawa kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akisisitiza kwamba hata wakati wa vita, serikali zina wajibu wa kuheshimu kanuni za ubinadamu na maadili ya kibinadamu.

Alieleza kuwa baada ya karne nyingi za vita na umwagaji damu katika Enzi za Kati, ubinadamu ulianza kutafakari kwa kina na hatimaye kuanzishwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa ili kuzuia uchokozi wowote dhidi ya mataifa. Pia miaka michache baadaye ikapitishwa Mikataba ya Geneva, inayolazimisha serikali kuzingatia misingi ya haki na kanuni za kibinadamu.

Ayatullah Mohaqqeq Damad alimwomba Papa amkumbushe rais wa Marekani mafundisho ya Nabii Isa (AS) na kumshauri kuepuka kumwaga damu zaidi ya watu wasio na hatia.

Mashambulizi ya Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Iran yalianza asubuhi ya Jumamosi, tarehe 28 Februari.

Kujibu uchokozi huo uliosababisha kuuawa shahidi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei, pamoja na makamanda kadhaa wa ngazi za juu wa kijeshi na mamia ya raia, wakiwemo watoto , Iran ilianzisha Operesheni Ahadi ya Kweli 4 (True Promise 4), ikifanya mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya malengo ya Israel na kambi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

4338638

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha