IQNA

Mufti Mkuu wa Libya awasisistizia tena Waislamu waiunge mkono Iran

13:48 - March 24, 2026
Habari ID: 3482084
IQNA-Mufti Mkuu wa Libya ametoa taarifa kuhusu mashambulizi na uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kwa mara nyingine amesisitiza kuwa: Ni wajibu kuwahami Waislamu pale vita vinapotokea baina ya Waislamu na makafiri.

Sheikh Sadiq al Ghariani amesema katika taarifa yake iliyoakisiwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwamba: “Katika Qur’ani Tukufu hakuna kitu kinachoitwa kutopendelea upande wowote. Ni wajibu kuwahami na kuwatetea Waislamu pale vita vinapotokea baina ya Waislamu na makafiri.”

Mufti Mkuu wa Libya anaendelea kusema: Mtu yeyote ambaye inapotokea vita baina ya Waislamu na makafiri huutaja msimamo wake kuwa ni wa “kutopendelea upande wowote” huwa miongoni mwa wale Qur’ani inasema ni vizabazabina baina ya huku na kule. Huku hawako na kule hawako.

Sheikh Al Ghariani amesema: “Miongoni mwa masomo na darsa zinazoona katika vita vya sasa ni kwamba Mustakbirina (mabeberu) wanapaswa kulipa gharama zake, bila kujali wana nguvu kiasi. Hii leo, Rais wa Marekani ameziomba nchi zote duniani zisaidie kufungua Lango Bahari la Hormoz na amepoteza matumaini.”    

Mufti Mkuu wa Libya amewahutubu Waislamu akisema: Acheni wajifunze kutokana na yale yanayojiri katika kambi za kijeshi za Marekani huko Ghuba ya Uajemi; uwepo wao umekuwa sababu ya kushambuliwa nchi walizokuwa wakidhani kwamba wanazilinda. Mtu yeyote anayekata izza na utukufu, basi utukufu uko kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini.”

4342438

captcha