IQNA

Mwanazuoni wa Misri asisitiza kufuata njia ya Shahidi Ayatullah Khamenei, atoa Fatwa ya kuunga mkono Iran

14:39 - March 03, 2026
Habari ID: 3482010
IQNA – Mwanazuoni mmoja wa Misri amempongeza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, na kusisitiza kwamba njia yake lazima iendelezwe na Umma ya Waislamu.

Sheikh Salamah Abdulqawi, mshauri wa zamani wa Waziri wa Mambo ya Awqaf nchini Misri, aliandika katika chapisho lake kwenye X kwamba Ayatullah Khamenei aliuawa shahidi katika shambulio baya la kigaidi lililofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni.

Akitoa mfano wa aya kutoka katika Qur’an Tukufu, alisema kuwa wanaume kama Ayatullah Khamenei wanastahili kufa shahidi .

Alisema kuwa Ayatullah Khamenei, ambaye alitumia maisha yake katika njia ya Jihad kwa ajili ya Msikiti wa Al-Aqsa, alitafuta shahada kwa dhati na akaipata.

Sheikh Abdulqawi aliandika katika chapisho jingine kwenye X kwamba kama watawala wa Kiarabu wangezitambua nguvu, furaha, na mafanikio wangeyapata, wangejitahidi kuunga mkono Iran.

“Fikiria tu kuhusu ulimwengu wa Kiarabu bila utawala huu haramu (Israel),” alieleza.

Wakati huo huo, Taasisi ya Fatwa na Utafiti ya Al-Azhar ilitoa taarifa, iliyotiwa saini na Sheikh Abdulqawi, ambayo inaona kuwa Wajibu (Wajib) kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na uchokozi wa Marekani na Israel.

Egyptian Scholar Stresses Following Path of Ayatollah Khamenei, Issued Fatwa on Support for Iran  

Taarifa hiyo ilisema: “Ni Wajibu kwa kila Muislamu kusimama upande wa Waislamu wengine dhidi ya makafiri, na imepigwa marufuku kuwasaidia makafiri au kuhalalisha vitendo vyao vya uchokozi au kufanya nao umoja.” Mwanazuoni huyo ameharamisha kuusaidia utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani.

Tawala fisadi na dhalimu za Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran kuanzia asubuhi ya Jumamosi, Februari 28.

Katika kujibu uchokozi huo wa Marekani na Israel, ambao umesababisha kufa shahidi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Seyed Ali Khamenei, pamoja na makamanda kadhaa wakuu wa kijeshi na mamia ya raia wakiwemo watoto wa shule, Iran imeanzisha Operesheni Ahadi ya Kweli 4, ikifanya mashambulizi makubwa ya makombora na droni dhidi ya malengo ya Israel na kambi za Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha