IQNA

Ayatullah Sistani alaani uvamizi wa Marekani dhidi ya Iran

17:42 - March 04, 2026
Habari ID: 3482013
IQNA – Kiongozi Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, amekemea kwa nguvu hujuma ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Iran, ambayo ilianza Jumamosi na hadi sasa imesababisha mamia kufa shahidi, wakiwemo watoto.

Ofisi ya Ayatullah al-Sistani, siku ya Jumatano, imekemea kwa nguvu shambulio la kijeshi la Marekani ambalo linaendelea dhidi ya Iran, ikisema kuwa mashambulio yaliyofanyika katika siku chache zilizopita yamewafanya raia wengi kuuawa shahidi, wakiwemo maafisa wa usalama wanaolinda nchi, idadi kubwa ya watoto na raia wengine wasio na hatia.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa ukubwa wa mzozo huo wa kijeshi umepanuka na kujumuisha nchi nyingine.

Kwenye taarifa hiyo, ofisi ya Ayatullah Sistani imetahadharisha  kuwa “uamuzi wa moja kwa moja wa mwanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuanzisha vita vya kimataifa dhidi ya nchi nyingine ya Umoja wa Mataifa ili kuweka masharti maalum au kuupindua mfumo wake wa kisiasa, mbali na kukiwa ni ukiukaji wa  mikataba ya kimataifa, ni jambo linalotoa mfano hatari sana.”

Taarifa hiyo imesema imeendelea kusema kuwa hatua kama hiyo itasababisha “matokeo mabaya kimataifa,” na yamkini kukaibuka machafuko makubwa na ya muda mrefu na hivyo kuongeza dhiki kwa watu wa eneo hilo sambamba na kudhuru maslahi ya wengine.

Kwa upande mwingine, taarifa hiyo imesema kuwa Ayatullah Sistani anakuemea kwa nguvu ‘vita hivi visivyo vya haki’” na kuwaka wale wote Waislamu na watu wenye fikra uhuru duniani kote kuvikiema na kuonyesha “mshikamano” na “watu waliodhulumiwa wa Iran.”

Kwa hitimisho, ofisi ya Ayatullah Sistani imesema kwa mara nyingine ametoa wwito kwa wahusika wote wa kimataifa, hasa nchi za Kiislamu, kufanya kila liwezekanalo kusitisha hujuma na  kufikia “suluhu haki na amani” ya kadhia ya nyuklia la Iran kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

3496640

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha