IQNA

Pezeshkian: Hujuma ya kijeshi ya Marekani-Israel haijatuachia chaguo lolote isipokuwa kujihami

12:37 - March 05, 2026
Habari ID: 3482014
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika ujumbe wake kwa viongozi wa nchi rafiki na majirani kwamba mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel yameiacha Iran bila chaguo lolote isipokuwa kujilinda.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Iran, IRNA, Masoud Pezeshkian, Rais wa Iran, ameandika kwenye mtandao wa X ujumbe ufuatao:

“Viongozi waheshimiwa wa nchi  rafiki na majirani, tulijaribu, kwa msaada wenu na kupitia diplomasia, kuepuka vita. Lakini mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na utawala wa Kizayuni hayajatuachia njia yoyote isipokuwa kujilinda.Tunaheshimu mamlaka yenu  ya kujitawala na bado tunaamini kuwa utulivu wa eneo hili unapaswa kudhaminiwa na nchi za eneo zenyewe.”

Vikosi vya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vinaendeleza operesheni za ‘Ahadi ya Kweli 4’ ikiwa ni katika kujibu uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ulioanzishwa Jumamosi.

Operesheni hizo za kijeshi za Iran zimeendelea kulenga ngome za kijeshi, kiuchumi na kisiasa za utawala wa Kizayuni wa Israel na vituo vya kijeshi na kijasusi vya Marekani katika ardhi za nchi za eneo.

4338411

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha