IQNA

Wabahrain waandama kuhimiza kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya Imam Khamenei

15:12 - March 03, 2026
Habari ID: 3482011
IQNA – Watu walifanya maandamano katika maeneo mbalimbali ya Bahrain, wakionyesha mshikamano wao na Iran na kutaka kulipiza kisasi kwa mauaji ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Ayatullah Seyed Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu Amrehemu).

Maelfu ya vijana wa Bahrain walishiriki maandamano hayo Jumatatu usiku, kulingana na mitandao ya kijamii.

Walilaani ushirikiano wa utawala wa kifalme nchini humo wa ukoo wa Al Khalifa na serikali ya Marekani katika mashambulizi dhidi ya Iran.

Kulingana na ripoti, mapigano makali yalizuka kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama vya Bahrain na vijana kadhaa wa Bahrain walikamatwa.

Wafuasi wa Muqawama nchini Bahrain wanasema wataendeleza maandamano yao hadi kuanguka kwa utawala wa kifalme wa Al Khalifa.

Ayatullah Seyed Ali Khamenei aliuliwa shahidi katika shambulio la Marekani na Israel dhidi ya ofisi yake mjini Tehran Jumamosi asubuhi.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili mapema, Baraza la Mawaziri la Iran lilituma salamu za rambirambi kwa Imam Zaman (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake), taifa Tukufu la Iran, na Umma ya Waislamu juu ya msiba huu mkuu na kutangaza siku 40 za maombolezo ya kitaifa.

Katika kujibu uchokozi wa Marekani na Israel, ambao umesababisha kuuawa kishahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, makamanda kadhaa wakuu wa kijeshi, na mamia ya raia wakiwemo watoto, Iran imeanzisha Operesheni Ahadi ya Kweli 4, ikifanya mashambulizi makubwa ya makombora na droni dhidi ya malengo ya Israel na kambi za Marekani katika eneo lote la Asia Magharibi.

4337893

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha