IQNA

Diplomasia

Afisa mwandamizi wa Iran asifu msimamo wa Mufti Mkuu wa Russia kuhusu matukio ya kimataifa

21:13 - December 07, 2024
Habari ID: 3479871
IQNA – Hujjatul Islam Mohseni Qomi, Mkuu wa Masuala ya Kimataifa katika Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, alisifu misimamo ya Mufti Mkuu wa Russia kuhusu masuala ya kimataifa na kikanda.

Hujjatul Islam Qomi alikutana na Mufti Mkuu wa Russia Sheikh Rawil Gaynetdin  wamekutana Moscow kujadili kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za kidini na kitamaduni. Balozi wa Iran nchini Russiai Kazem Jalali, mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Moscow, na viongozi kadhaa wa kidini na kitamaduni kutoka nchi hizo mbili pia walihudhuria mkutano huo.

Hujjatul Islam Qomi amesema kwamba Mufti Mkuu wa Russia na Idara ya Dini ya Kiislamu ya nchi hiyo wamechukua misimamo ya kibinadamu, Kiislamu, na yenye thamani kuhusu masuala kama Gaza na jinai za  Israel huko Palestina na Lebanon, ambayo inapaswa kupongezwa. Pia alisifu jukumu la Mufti Mkuu katika kuleta ukaribu wa shule za mawazo za Kiislamu nchini Russia.

Hujjatul Islam Qomi alisema kwamba Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na rais wa Iran wanasisitiza maendeleo na kuimarisha uhusiano wa pande mbili na Russia na kwamba mahusiano hayo yanaendelea kupanuka kwa juhudi za Rais wa Russia Vladimir Putin. Sheikh Rawil Gaynetdin, kwa upande wake, alituma salamu zake kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Alisema kwamba chini ya uongozi wa busara wa Ayatullah Seyed Ali Khamenei na rais wa Russia na Iran nchi mbili zitapata ushindi dhidi ya wapinzani wao.

Pia alikumbuka ziara ya rais wa zamani wa Iran, Ebrahim Raisi, katika Msikiti wa Jamia wa Moscow na kuitaja kama chanzo cha heshima kwa Idara ya Dini ya Kiislamu ya Russia.

3490961

 

Kishikizo: iran russia mufti
captcha