IQNA

Wanazuoni wa Yemen wasema kusaidia Iran na Hizbullah ni wajibu wa kidini

12:15 - March 06, 2026
Habari ID: 3482019
IQNA —Chama cha Wanazuoni wa Yemen kimesema kuwa kuisaidia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ni wajibu wa kidini (wajib).

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi, chama hicho kimelaani vikali uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya Iran na Lebanon.

Taarifa hiyo imesisitiza kwamba kuwasaidia ndugu wa Kiislamu nchini Iran na wapiganaji wa Hizbullah nchini Lebanon dhidi ya maadui waovu zaidi miongoni mwa maadui wa Mwenyezi Mungu ni wajibu wa kidini na jukumu la Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha habari cha Al‑Maseerah, chama hicho pia kimesisitiza kuwa katika hali ya sasa kubaki bila kuchukua msimamo hakukubaliki.

Marekani na utawala wa Israel walianza mashambulizi dhidi ya Iran kuanzia asubuhi ya Jumamosi, tarehe 28 Februari.

Kwa kujibu mashambulizi hayo, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei pamoja na makamanda kadhaa wa juu wa kijeshi na mamia ya raia, Iran imeanzisha Operesheni “Ahadi ya Kweli 4”, ikitekeleza mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya malengo ya Israel na vituo vya Marekani katika eneo hilo.

3496651

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha