IQNA

Farhan Haq: Hujuma ya kijeshi dhidi ya Iran inakiuka hati ya Umoja wa Mataifa

12:45 - March 05, 2026
Habari ID: 3482015
IQNA-Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuwa hujuma ya kijeshi yaliyotumika na Marekani na Israel dhidi ya Iran inakiuka Kanuni za Umoja wa Mataifa.

Farhan Haqq ameyasema katika mazungumzo na Televisheni ya Al Jazeera na kuongeza kuwa: “Uhalali wa kimataifa unatokana na Kanuni za Umoja wa Mataifa, na wote wanapaswa kuheshimu msingi huu.”

Ameongeza kuwa, sasa Umoja wa Mataifa umetoa mkazo mkubwa wa kuzuia kushadidi kwa kwa migogoro, kuhakikisha usalama wa raia, kuzuia hali mbaya ya binadamu, na kupunguza madhara kwa uchumi wa kimataifa.

Farhan Haqq, ameelezea wasiwasi mkubwa wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezeka kwa tishio la migogoro katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) na kupanuka kwa uwanja wa vita.

Msemaji huyo, akizungumzia mchakato wa Kimataifa, alibainisha kuwa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ana wasiwasi mkubwa wa kuhusu kuongezeka kwa tishio, vifo vya raia, na matokeo ya hatari ya vita kwa wananchi wa eneo hilo. Kuhusu mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, Farhan Haqq amesisitiza kuwa Katibu Mkuu amesema mara nyingi kuwa Kanuni ya Umoja wa Mataifa unapinga matumizi ya nguvu au tishio la nguvu dhidi ya nchi kwani ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Kwa upande wa mpango wa nyuklia ya Iran, Haqq amesema wazi kuwa njia pekee ya kutatua suala hili ni kurudi kwenye meza ya mazungumzo. Pia, ametoa onyo kali kwamba endapo sera za kijeshi zitaendelea, basi kutashuhudiwa uharibifu mkubwa zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Haqq ameongeza kuwa, hali hii inaweza kuathiri vibaya  uchumi wa dunia yote, na siyo tu uchumi wa eneo la Mashariki ya Kati.

4338242

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha