
Imam Khamenei aliuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel tarehe 28 Februari sawa na 10 Ramadhani, sambamba na kuanza hujuma ya kichokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kitovu cha mijumuiko hiyo ya Arubaini ni mji mkuu wa Iran, Tehran, ambapo waombolezaji walianza matembezi yao kutoka Medani ya Jamhuri ya Kiislamu kuelekea mahali pa kuuawa shahidi kwa Imam Shahidi.
Wananchi waliokuwa na huzuni ya shahada ya Kiongozi wa Umma , kutoka makundi na mitazamo mbalimbali, vijana kwa wazee, wengi wao wakiwa pamoja na familia zao , wameshiriki wakiwa wameshika picha za Kiongozi Shahidi wa Umma pamoja na bendera za Iran zilizoandikwa aya tukufu: “Hakika Mola wangu yu pamoja nami; ataniongoza” na “Wala msilegee wala msihuzunike; ninyi ndio mtakaokuwa juu,” pamoja na bendera za Harakati ya Hizbullah.
Wananchi walioshiriki wameendelea kutoa wito wa kulipiza kisasi cha damu ya Imam Khamenei, makamanda na wananchi waliouawa shahidi, wakiwemo watoto wa shule.
Katika njia ya maombolezo, miongoni mwa ratiba za hafla hiyo kulikuwa na usomaji wa Qur’ani Tukufu na kasida za maombolezo.
Waombolezaji hao pia walisoma kwa pamoja Suratul Yasin na kuitoa kama zawadi kwa roho ya Kiongozi Shahidi.
Kiongozi huyo mwenye hekima alitumia maisha yake yote yenye baraka kwa ajili ya kuinua neno la haki, kulinda misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu, na kulitumikia kwa ikhlasi taifa hili kubwa sambamba na kutetea watu wanyonge kote duniani.

Leo, katika siku ya arubaini tangu kupaa kwake kwenye daraja ya juu ya kiroho, wananchi waaminifu na watiifu wa Iran wameonyesha kwa mahudhurio yao makubwa na ya kuvunja moyo wa maadui kwamba hawalii tu kwa huzuni ya kumpoteza kiongozi wao, bali pia wamesimama imara zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika ahadi yao ya kudumisha njia na malengo yake.
Wananchi wa Tehran pamoja na kutoka majimbo mengine ya nchi wamehudhuria kwa hisia na hamasa kubwa, hasa baada ya siku arubaini za mapambano dhidi ya maadui ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya kinyama dhidi ya Iran.
Aidha, siku ya Ijumaa, kutafanyika hafla za kumuenzi Imam Shahidi katika maeneo ya kuswali Swala ya Ijumaa katika miji yote ya Iran.
Miongoni mwa mipango mingine ya Arubaini ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ni pamoja na khitma ya usomaji wa Suratul Fath kwa nia ya ushindi wa taifa la Iran na kambi ya muqawama.
4345296/