TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeitaja tetesi iliyoenea katika vyombo vya habari vya Kizayuni kuhusu jitihada za utawala huo za kufikia makubaliano ya usitishaji vita ya muda mrefu na Ukanda wa Ghaza kuwa ni propaganda za uchaguzi.
Habari ID: 3472257 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/05
Kamanda Mkuu wa IRGC
TEHRAN (IQNA)- Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) mezungumzia mwamko na muono wa mbali wa wananchi wa Iran katika matukio ya hivi karibuni humu nchini na kusisitiza kuwa, wiki zilizopita, wananchi wa Iran walitoa pigo jingine kubwa kwa mabeberu hususan Marekani.
Habari ID: 3472256 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/04
TEHRAN (IQNA) –Harakati ya Kiislamu Nigeria (INM) imesema hatua ya serikali ya nchi hiyo kuendelea kumshikilia Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake ni ukiukwaji wa wazi wa sharia.
Habari ID: 3472255 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/04
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Ulaya na Marekani hazina azma ya kurejesha amani huko Yemen bali pande hizo zinafuatilia kuuza silaha zao.
Habari ID: 3472254 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/03
TEHRAN (IQNA) – Washindi wa Duru ya 26 ya Mashindano ya Qur'ani ya Sheikh Jassim bin Mohammed bin Thani nchini Qatar wametunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika Jumatatu.
Habari ID: 3472253 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/03
TEHRAN (IQNA)- Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani Jumatatu ametembelea msikiti katika mji wa Penzberg na kutoa wito wa kuwepo hali ya kuheshimiana baina ya wafuasi wa dini mbali mbali.
Habari ID: 3472252 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/03
TEHRAN (IQNA) – Adhana imesikika kwa mara ya kwanza katika msikiti mmoja mkongwe nchini kaskazini mwa Macedonia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 107.
Habari ID: 3472251 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/02
TEHRAN (IQNA) Bunge la Iraq lililokutana kwa kikao cha dharura kilichofanyika Jumapili limeukubali uamuzi uliochukuliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Adil Abdul-Mahdi wa kujiuzulu wadhifa wake huo.
Habari ID: 3472250 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/02
TEHRAN (IQNA) – Timu ya watu 40 wakiwemo wakalimani na wanazuoni wa Uislamu wanatazamiwa kuanza kuandika tarjumi mpya ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kirussia.
Habari ID: 3472249 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/02
TEHRAN (IQNA) – Wanawake nchini Uzbekistan wameshiriki katika mashindano ya Qur'ani ambaye yamefanyika hivi karibuni katika mji mkuu, Tashkent.
Habari ID: 3472247 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/01
TEHRAN (IQNA) - Tarehe 29 Novemba iliadhimishwa kote duniani kama Siku ya Kimataifa ya Kuonesha Mshikamano na Taifa la Palestina
Habari ID: 3472246 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/01
TEHRAN (IQNA) – Nakala ya kale zaidi ya Qur'ani Tukufu nchini China imewekwa katika maonyesho ya umma kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Habari ID: 3472245 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/01
Leo Katika Historia
TEHRAN (IQNA) - Katika siku kama ya leo miaka 31 iliyopita, aliaga dunia katika mji wa Cairo Misri, Sheikh Abdul-Basit Abdul-Samad, mmoja wa waalimu na maqarii wakubwa wa Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3472244 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/30
Waziri Mkuu wa Malaysia
TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa Malaysia Dakta Mahathir Mohammad amesema Waislamu wanapaswa kuwa na tabia njema na maadili bora ili kuwavutia wasiokuwa Waislamu katika Uislamu.
Habari ID: 3472243 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/30
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yamepengwa kufanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad mwakani.
Habari ID: 3472242 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/30
TEHRAN (IQNA) – Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa wito kwa kuwepo jitihada za pamoja baina ya Russia na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) katika kukabiliana na changamoto za kimataifa.
Habari ID: 3472241 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/29
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA) -Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kulikuwa na mpango hatari nyuma ya wazua ghasia za hivi karibuni nchini Iran ambapo ghasia hizo ziliratibiwa na uistikbari wa dunia miaka miwili iliyopita sambamba na kugawa silaha na kutoa mafunzo.
Habari ID: 3472240 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/29
TEHRAN (IQNA)- Msikiti umeteketezwa moto mjini Chicago nchini Marekani katika tukio linaloaminika kutekelezwa na magadidi wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Habari ID: 3472239 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/29
TEHRAN (IQNA) – Miaka mine iliyopita, uliwekwa msingi wa Msikiti wa Abdülhamid II nchini Djibouti na sasa mradi huo umekamilika.
Habari ID: 3472238 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/28
TEHRAN (IQNA) – Serikali za Iran na Iraq zimelaani hujuma dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mtakatifu wa Najaf huku serikali ya Iraq ikisema hujuma hiyo imelenga kuvuruga uhusiano wa kihistoria wa nchi hizi mbili jirani.
Habari ID: 3472237 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/28