IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani ya Sheikh Jassim Qatar watunukiwa Zawadi

19:10 - December 03, 2019
Habari ID: 3472253
TEHRAN (IQNA) – Washindi wa Duru ya 26 ya Mashindano ya Qur'ani ya Sheikh Jassim bin Mohammed bin Thani nchini Qatar wametunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika Jumatatu.

Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar Ghaith bin Mubarak Al Kuwari alikuwa mgeni wa heshima katika sherehe hiyo iliyofanyika katika mji mkuu, Doha.

Kulikuwa na kategoaria kadhaa za mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, Tajweed na Tarteel. Mashindano hayo yalikuwa na kategoria ya raia wa Qatar na kategoria ya raia wa kigeni wanaoishi Qatari.

Walioshika nafasi ya kwanza walipata zawadi ya fedha taslimu Riali za Qatar (QR) 100,000 huku walioshika nafasi za pili wakipata QR 85,000 huku walioshika nafasi za tatu wakipata QR 70,000, nafasi za nne QR 60,000 na nafasi za tano QR 50,000.

Mashindano hayo ya kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu nchini Qatar.   Mchujo wa mashindano hayo ulifanyika Novemba 16-21 na fainali ikafanyika kuanzia Novemba 25-26.

3861426

captcha