iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA) – Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa na asasi zingine za kieneo kuitangaza Machi 25 kama Siku ya Kimataifa ya Mshikamano katika Kukabiliana na Chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3472236    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/28

Kiongozi Muadhamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshukuru harakati ya wananchi wengi wa taifa la Iran katika kipindi cha wiki moja iliyopita na kusisitiza kuwa kwa harakati hiyo wananchi wa Iran wamesambaratisha njama kubwa, hatari sana na iliyoratibiwa.
Habari ID: 3472235    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/27

TEHRAN (IQNA) – Mufti wa Waislamu wa eneo la Volgograd Oblast nchini Russia amesisitiza ulazima wa kukombolewa mji Mtakatifu wa Quds, sehemu uliko Msikiti wa Al Aqsa na kusema kutetea Quds Tukufu na Palestina kunapaswa kuwa kadhia muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa.
Habari ID: 3472234    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/27

TEHRAN (IQNA) – China imetoa taarifa na kupinga madai ya kimataifa kuwa imewaweka Waislamu wa mkoa wa Xinjiang katika kambi maalumu kwa lengo la kuwabadilisha itikadi zao.
Habari ID: 3472232    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/26

TEHRAN (IQNA) –Jeshi la kujitolea la wananchi nchini Iran maarufu kama Basiji limezindua chekechea 620 mpya za Qur’ani Tukufu kote nchini.
Habari ID: 3472231    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/26

TEHRAN (IQNA) – Pakistan imelaani vikali hatua ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na imemkabidhi balozi wa Norway mjini Islamabad malalamiko sambamba na kupanga kuwasilisha malalamiko katika Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC.
Habari ID: 3472230    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/25

TEHRAN (IQNA) –Binti Muislamu mwenye kuvaa Hijabu, Khadijah Mellah, ametangazwa kuwa Mwanamichezo Bora Msichana wa mwaka nchini Uingereza kufuatia ushindi wake katika mashindano ya mbio za farasi ya Kombe la Magnolia.
Habari ID: 3472228    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/24

TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kimataifa cha Fatwa katika Chuo cha Al Azhar nchini Misri kimetoa taarifa na kusema vazi la Hijabi ni faradhi kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3472227    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/23

TEHRAN (IQNA)- Manispaa ya Mji wa Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imetangaza kuwa watu milioni moja wameitembelea Bustani ya Qurani tangu ifunguliwe mjini humo mwezi Machi mwaka huu.
Habari ID: 3472226    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/22

TEHRAN (IQNA) - Shirika la Kiislamu la Elimu Sayansi na Utamaduni (ISESCO) limetangaza kuwa linaendesha shughuli 50 za Qur'ani Tukufu kila mwaka.
Habari ID: 3472225    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/21

TEHRAN (IQNA)- Waislamu duniani wameendelea kulaani hatua ya Marekani kubadili msimamo na kuanza kuunga rasmi hatua iliyo kinyume cha sheria ya Israel ya kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina.
Habari ID: 3472224    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/20

TEHRAN (IQNA) - Kitendo cha kuichoma moto Qur'an Tukufu kilichojiri katika mkusanyiko mmoja wa maandamano hivi karibuni nchini Norway kimeendelea kulaaniwa.
Habari ID: 3472223    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/20

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelihutubu taifa la Iran pamoja na marafiki na maadui wa mapinduzi na kusisitiza kuwa, wote, wakiwemo marafiki na maadui wa mapinduzi wafahamu kuwa, kuhusiana na medani ya kijeshi, kisiasa na kiusalama -kama vitendo vya machafuko na uharibifu vilivyotokea hivi karibuni hapa nchini ambavyo havikufanywa na wananchi wa kawaida- tumemuacha nyuma adui na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu tutamshinda adui huyu pia katika medani ya vita vya kiuchumi.
Habari ID: 3472222    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/20

TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Kituo cha Kiislmau cha Al Azhar nchini Misri, Sheikh Ahmed el Tayeb amekutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, Ijumaa mjini Vatican.
Habari ID: 3472221    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/18

TEHRAN (IQNA) – Washiriki katika Mkutano wa Pili wa Viongozi wa Kidini Duniani umefanyika huko Baki katika Jamhuri ya Azerbaijan ambapo washiriki wamesisitiza kuhusu ulazima wa kuheshimu uwepo wa dini mbali mbali sambamba na kuendeleza vita dhidi ya ugaidi.
Habari ID: 3472220    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/18

TEHRAN (IQNA) – Mufti Shawqi Allaam amesema Uislamu ni dini ya ustahamilivu na rehema na inataka watu waishi pamoja kwa amani na wawe na mazungumzo baina yao.
Habari ID: 3472219    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/18

TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa 33 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umemalizika mjini Tehran Jumamosi usiku.
Habari ID: 3472218    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/17

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuondolewa Israel kuna maana ya kuondolewa utawala bandia wa Kizayuni na mahala pake kuchukuliwa na serikali iliyochaguliwa na wamiliki wa asili wa Palestina ambao ni Waislamu, Wakristo na Mayahudi.
Habari ID: 3472216    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/15

TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko mstari wa mbele katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani katika kuwatetea watu wa Palestina.
Habari ID: 3472215    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/14

TEHRAN (IQNA)- Makamanda wawili wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina wameuawa aktika hujuma mpya za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3472213    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/13