iqna

IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA)-Filamu ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii imemuonyesha mtoto mdogo wa Kiislamu akiondolewa kwa nguvu katika familia yake ya Kiislamu na maafisa wa "huduma za ulinzi wa watoto" na askari polisi wa Ujerumani kwa sababu wazazi wake wanadaiwa kumfundisha kwamba mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja hayakubaliki katika Uislamu.
Habari ID: 3476935    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/30

Waislamu Kanada
TEHRAN (IQNA) - Shirika moja la Waislamu wa Kanada (Canada) limelaani hatua ya polisi wa Edmonton ya kumkamata kwa mabavu na vurugu Mwislam mwenye asili ya Afrika wiki iliyopita.
Habari ID: 3476926    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/28

Hali ya Waislamu
TEHRAN (IQNA) – Kundi la wanafunzi Waislamu wanaendelea kupigania haki yao ya kuwa na mahali pa ibada huko Daegu, Korea Kusini, huku kukiwa na unyanyasaji wa chuki dhidi ya Uislamu katika eneo hilo.
Habari ID: 3476923    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/27

Waislamu India
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya India yenye misimamo ya kufurutu ada imefuta historia ya watawala wa Kiislamu katika vitabu vya masomo na kuzidi kuthibitisha kwamba, inafuatilia kwa nguvu zote siasa za kukabiliana na Waislamu pamoja na historia yao.
Habari ID: 3476921    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/27

Njia ya Haki
TEHRAN (IQNA) – Mzee mmoja ambaye alifika Msikitini kulalamika kuhusu kelele katika eneo hilo la ibada huko Australia hatimaye alisilimu baada ya kukaribishwa kwa ukarimu na waumini waliokuwa Msikitini hapo.
Habari ID: 3476918    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/26

Idul Fitr
TEHRAN (IQNA) - Kwa watoto katika jamii ya Waislamu wa eneo la St. John nchini Kanada, Jumamosi ilikuwa siku ambayo walijumuika pamoja baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3476904    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/23

Waislamu Marekani
TEHRAN (IQNA) – Jiji la Minneapolis limekuwa jiji la kwanza kubwa la Marekani kuruhusu utangazaji bila vikwazo wa wito wa Waislamu wa Sala yaani Adhana kwa sauti inayosikika nje ya msikiti mara tano kwa siku mwaka mzima.
Habari ID: 3476872    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/15

TEHRAN (IQNA) - Baraza la Mahusiano ya Marekani na Uislamu (CAIR) lilitoa ripoti Jumanne iliyoangazia matukio ya kitaifa ya malalamiko ya haki za kiraia yaliyofanywa na Waislamu Wamarekani mwaka 2022 ambayo yalionyesha kupungua kwa 23%.
Habari ID: 3476861    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/13

Waislamu katika Ramadhani
TEHRAN (IQNA)- Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Ethiopia limefanya hafla kubwa zaidi ya Iftar au Futari katika uwanja wa Al-Thaura mjini Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo, wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3476844    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/10

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Biashara wa Kanada, Mary Ng amelaani shambulio la chuki dhidi ya Uislamu lililolenga msikiti mmoja eneo la Markham, Ontario wakati mtu mmoja alipovunjia heshima nakala ya Qur'ani Tukufu na kujaribu kuwashambulia waumini kwa gari.
Habari ID: 3476842    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/10

Waislamu Uingereza
TEHRAN (IQNA) - Mamia walikusanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa kifahari wa Royal Albert Hall huko London kama sehemu ya futari ya wazi - tukio la kijamii wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3476841    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/09

Chuki dhidi ya Uislamu
TEHRAN (IQNA) – Marefa nchini Ufaransa wameamuriwa na shirikisho la soka la nchi hiyo kutositisha mechi ili kuwaruhusu wachezaji Waislamu kufuturu katika mwezi wa Ramadhani.
Habari ID: 3476794    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/01

Waislamu Afrika
TEHRAN (IQNA)- Idadi kubwa ya Waislamu waliyoyakimbia makazi yao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na ghasia na machafuko, wanataabika na kuteseka katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3476791    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/31

Mwezi wa Ramadhani
TEHRAN (IQNA) – Wauguzi kadhaa wasio Waislamu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wanafunga kula na kunywa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vile wanataka kuonyesha mshikamano na wenzao Waislamu katika mwezi huu.
Habari ID: 3476785    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/30

Chuki dhidi ya Waislamu
TEHRAN (IQNA)- Shirika moja lisilo la kiserikali imeripoti kuwa, wanawake Waislamu wanaovaa vazi la staha la Hijabu nchini Austria wanakabiliwa ubaguzi na mashambulio ya wenye chuki dhidi ya Uislamu ikilinganishwa katika nchi hiyo ya Ulaya.
Habari ID: 3476783    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/30

Uhalifu
TEHRAN (IQNA) - Watu wawili wameuawa katika shambulio la kudunga visu kwenye Kituo cha Waislamu cha Ismaili katika jiji kuu wa Ureno, Lisbon.
Habari ID: 3476781    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/29

Ukarimu katika Mwezi wa Ramadhani
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zimezindua kampeni ya ukarimu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yenye lengo la kutoa msaada wa milo bilioni moja kwa wale wanaohitaji kote kote duniani.
Habari ID: 3476770    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/27

Wanamichezo Waislamu
TEHRAN (IQNA) - Mchezaji soka maarufu wa Bosnia na Herzegovina Anel Ahmedhodzic ameusifu mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni mwezi wa kumwabudu Mwenyezi Mungu na kuleta jamii pamoja.
Habari ID: 3476768    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/27

Harakati za Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) nchini Libya imezindua Mus’haf (nakala ya Qur’ani Tukufu) iliyochapishwa na Shirika la Wakfu la nchi hiyo.
Habari ID: 3476734    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/20

Wanamichezo Waislamu
TEHRAN (IQNA)- Mchezaji chipukizi wa akademia ya Soka ya klabu maarufu ya Manchester United nchini Uingereza amewavutia wengi baada ya klipu yake akiwa anasema Qur'ani Tukufu kuenea mitandaoni. Katika kilipu iliyosambazwa na kaka yake, Amir Ibragimov mwenye umri wa miaka 15 anaonekana akisoma sehemu ya Surah Al-Furqan ndani ya Kituo cha Trafford mjini Manchester nchini Uingereza
Habari ID: 3476715    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/16