IQNA

Waislamu Marekani

Mmarekani aliyelenga kuwagonga Waislamu kwa gari afikishwa kizimbani

15:01 - August 11, 2023
Habari ID: 3477416
WASHIGNTON, DC (IQNA) - Mwanamume mmoja ameshtakiwa kwa uhalifu wa chuki baada ya kushambulia kundi la Waislamu katika bustani moja huko California, Marekani siku ya Jumatatu.

Robert Avery, amaye pia ni mhalifu wa ngono, aliripotiwa kupiga kelele za kibaguzi na kutishia "kuwapiga risasi na kuwalenga kwa mabomu" Waislamu, ambao walikuwa na asili ya Asia Kusini na walikuwa takriban 30. Pia inadaiwa aliendesha gari aina ya Honda Insight 2012 kuelekea Waislamu hao katika Bustani ya  Heron Landing huko Rancho Cordova, California, kwa lengo la kuwagonga na kuwadhuru kimwili.

Mshukiwa alijisalimisha kwa mamlaka karibu saa 12 baada ya tukio hilo. Anakabiliwa na mashtaka ya kushambulia kwa silaha mbaya, kutoa vitisho vya uhalifu, na uhalifu wa chuki.

Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR) katika Bonde la Sacramento na California ya kati lilisifu watekelezaji sheria wa eneo hilo kwa hatua yao ya haraka.

Layli Shirani, wakili mkuu wa haki za kiraia katika baraza hilo, alisema: "Tunashukuru mamlaka za utekelezaji wa sheria za mitaa kwa hatua yao ya haraka ya kumpeleka mshukiwa kizuizini na tunazitaka mamlaka za shirikisho kufikiria kuleta mashtaka ya uhalifu wa chuki kwa shambulio hili linaloonekana kulenga ya jamii ya wachache.”

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni iliyochapishwa na Taasisi ya Sera na Maelewano ya Kijamii (ISPU), kuenea kwa ubaguzi dhidi ya Waislamu nchini Marekani hakujaonyesha mabadiliko makubwa. Takwimu kutoka kwa ripoti hiyo zinaonyesha kuwa takriban asilimia 60 ya Waislamu wameripoti kukabiliwa na ubaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ukiwemo mwaka wa hivi majuzi zaidi uliofanyiwa utafiti.

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na matukio mashuhuri ya unyanyasaji uliolengwa kwa jamii za Waislamu katika Amerika ya Kaskazini na ulimwengu wa Magharibi kwa ujumla. Tukio moja kama hilo lilitokea mwaka wa 2017 wakati msikiti katika Jiji la Quebec  Kanada ulishambuliwa, na kusababisha hasara ya kusikitisha ya Waislamu sita wasio na hatia.

Vile vile, mnamo 2019, mtu mwenye bunduki alishambuliwa Waislamu msikitini wakati wa sala ya Ijumaa huko New Zealand, na kuwaua zaidi ya waumini 50 wa Kiislamu. Matukio haya yanadhihirisha hali ya kutisha ya mashambulizi yanayochochewa na  chuki za kidinidini dhidi ya Waislamu katika jamii za Magharibi.

/3484724

Habari zinazohusiana
Kishikizo: marekani waislamu cair
captcha