IQNA

Uchambuzi

Miongo miwili baada ya hujuma za Septemba 11, 2001

20:21 - September 11, 2023
Habari ID: 3477585
TEHRAN (IQNA)- Miaka 22 imepita tangu baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 katika miji ya New York na Washington, tukio ambalo liliathiri sio Marekani pekee, bali karibu dunia nzima.

Katika mashambulizi hayo ya kigaidi, ambayo yanatambuliwa kuwa tukio kubwa zaidi la kigaidi katika historia ya Marekani, karibu watu elfu tatu waliuawa.

Kwa mujibu wa maelezo rasmi ya serikali ya Marekani, kundi la kigaidi la Al-Qaida na Usama bin Laden, kiongozi wa kundi hilo wakati huo, walihusika na mashambulizi dhidi ya majengo pacha ya World Trade Center mjini New York na jengo kubwa la Wizara ya Ulinzi ya Marekani huko Washington. Ni muhimu kukumbuka kuwa, kundi hili la kigaidi liliundwa na Wamarekani wakati wa vita na Umoja wa Kisovieti baada ya Afghanistan kukaliwa kwa mabavu na Urusi; na Bin Laden mwenyewe alipewa mafunzo katika kambi za siri za shirika la ujasusi la Marekani, CIA. Hata hivyo matukio ya baada ya kuondoka vikosi vya jeshi la Sovieti huko Afghanistan yaliwapambanisha uso kwa uso bwana na mtwana wake, yaani Marekani na kundi ililounda na kulianzisha yenyewe la al Qaida, ambalo baadaye lilifanya shambulio la kigaidi la kutisha dhidi ya bwana na muundaji wake. 

Marekani iliua watu zaidi ya milioni 4.5 baada ya Septemba 11

Pamoja na hayo yote inatupasa kuelewa kuwa, mashambulizi ya kigaidi ya Al-Qaida huko Marekani mnamo Septemba 11, 2001 hayakuwa mwisho wa uhusiano kati ya pande hizo mbili. Wamarekani walianzisha mashambulizi eti ya kulipiza kisasi cha Septemba 11 kwa anwani ya "Vita dhidi ya Ugaidi", ambayo wahanga wake walikuwa mara elfu kadhaa zaidi ya wale wa matukio yenyewe ya Septemba 11, 2001. Ripoti iliyochapishwa mwaka 2023 ilionyesha kuwa, vita vilivyoongozwa na Marekani baada ya shambulio la 9/11 viliua watu wasiopungua milioni 4.5 na kuwalazimisha mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao. Kwanza, na katika moja ya vita visivyokuwa na mlingano katika historia, Marekani, na washirika wake katika NATO na nchi nyingine kadhaa, waliishambulia Afghanistani, na baada ya kupindua serikali ya Taliban, walianza kuitawala nchi hiyo iliyoharibiwa na vita kwa kipindi cha miaka 20. 

Kisha ilikuwa zamu ya Iraq, ambayo watawala wake hawakuhusika katika mashambulizi ya Septemba 11, 2001. Hata hivyo, Wamarekani wenye kiu ya umwagaji damu waliivamia Iraq kwa mara ya pili chini ya bendera ya "vita vya mapema" na kuikalia kwa mabavu nchi hiyo baada ya kupindua serikali yake. Kutokana na shaghalabaghala iliyosababishwa na uvamizi wa Marekani nchini Iraq na kuikalia kwa mabavu nchi hiyo, kuliibuka kundi la kigaidi katili zaidi kuliko al-Qaida, lililojulikana kwa jina la ISIS au Daesh, katika nchi ya Iraq na kisha Syria. Kundi hili pia lilifanya ukatili wa kutisha katika eneo la Asia Magharibi; Na wakati huo huo matawi ya al-Qaida barani Afrika yalikuwa bado yanajihusisha na uhalifu na mauaji ya watu wasio na hatia.

Marekani imechochea zaidi ugaidi

Sasa ikiwa imepita miaka 22 tangu tukio la kigaidi la Septemba 11, 2001, inabainika kuwa "vita dhidi ya ugaidi" ambayo ilianzishwa na Wamarekani kwa madai ya kuangamiza ugaidi duniani, yenyewe ilichochea zaidi ugaidi duniani. Njia isiyofaa ya Wamarekani katika kushughulikia makundi ya kigaidi, ambayo mara nyingi iliambatana na mauaji ya raia wasio na hatia, ilitayarisha mazingira ya kuibuka hasira za umma miongoni mwa raia ambayo yalitumiwa vibaya na makundi ya kigaidi. Kwa maneno mengine ni kuwa, ukatili wa Wamarekani ulipelekea kuimarika shughuli za makundi ya kigaidi, ambazo pia zilizidisha ukatili na unyama wa Wamarekani. Wahanga wa mzunguko huo wa ukatili walikuwa wanawake, wanaume na watoto ambao walipoteza maisha, kuharibu mali na hadhi za waliobakia hai na kundamwa na mashaka mengi katika jitihada za kuepuka kifo.

Wakati huo huo raia wa Marekani pia walilipa gharama kubwa ya mienendo ya serikali ya nchi yao katika kalibu ya "vita dhidi ya ugaidi". Ijapokuwa baada ya Septemba 11, 2001, hakukutukia tukio kubwa kama mashambulio ya kigaidi la New York na Washington huko Marekani, lakini vikundi vya kigaidi vya ndani ya Marekani vilistawi na kupanuka zaidi kutokana na vyombo vya ujasusi na usalama vya nchi hiyo kuelekeza mazingatio kwenye vitisho vya ugaidi wa kigeni. Sasa inasemekana kwamba, usalama wa Wamarekani unatishiwa zaidi na makundi yenye itikadi kali za kibaguzi ya ndani kuliko vikundi kama Al-Qaida na Daesh.

Jambo lisilo na shaka ni kuwa, ulimwengu umekuwa mahali pasipo na usalama zaidi baada ya Septemba 11, 2001, na Wamarekani wana nafasi na mchango mkubwa katika kujitokeza hali hii.

Hali ya Waislamu Marekani

Waislamu nchini Marekani bado wanakabiliwa na chuki na ubaguzi, miongo miwili baada ya mashambulizi ya 9/11. Hayo ni kulingana na shirika kubwa la Kiislamu nchini humo.
"Baada ya miaka 22, kwa bahati mbaya, chuki dhidi ya Uislamu imekita mizizi na kuwa sehemu ya muundo wa ubaguzi wa rangi uliopo katika sehemu za nchi yetu," alisema Hussam Ayloush, afisa mkuu mtendaji wa sura ya California ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR-CA). )

Ayloush anasema kwamba karibu milioni moja kati ya Waislamu wanaokadiriwa kufikia milioni tano wanaoishi Marekani wanaishi katika jimbo la California na kudokeza kwamba unyanyasaji na chuki dhidi ya jamii ya Kiislamu zimesalia kuwa nyingi miongo kadhaa baada ya 9/11.

"Zaidi ya 50% ya wanafunzi Waislamu huko California wanakabiliwa na aina fulani ya unyanyasaji wa maneno na kimwili katika shule za umma kwa sababu tu ya kuwa Waislamu" alisema Ayloush.

3485123

Habari zinazohusiana
Kishikizo: cair marekani waislamu 9/11
captcha