ayatullah khamenei - Ukurasa 2

IQNA

IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ametaja Idul-Ghadir, ambayo mwaka huu inaangukia tarehe 14 Juni, kuwa ni siku ya kipekee kwa Umma wa Kiislamu.
Habari ID: 3480826    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/12

Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mahujaji wa Beitul Haram mjini Makka
IQNA-Katika ujumbe wake kwa Mahujaji wa Beitul Haram katika mji mtakatifu wa Makka, Ayatullah Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Serikali za Kiislamu zinapaswa kufunga njia zote za kuusaidia utawala wa Kizayuni, na kwamba wananchi nao wanapasa kuziwajibisha serikali zao katika kufikia lengo hilo.
Habari ID: 3480791    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/05

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema urutubishaji wa urani ndio ufunguo wa suala la nyuklia la Iran, akipuuzilia mbali pendekezo la Marekani kwa Tehran la kusimamisha kikamilifu urutubishaji wa madini hayo (ya urani).
Habari ID: 3480785    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/04

IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemsifu Shahidi Rais Ebrahim Raisi kama mtumishi wa umma aliyejitolea, ambaye unyenyekevu wake na kujituma bila kuchoka kwa ajili ya watu vilimtofautisha na wengine.  
Habari ID: 3480714    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/20

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amekosoa matamshi ya hivi karibuni ya Rais Donald Trump wa Marekani na kuyataja kuwa ni "fedheha" kwa taifa la Marekani.
Habari ID: 3480694    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/17

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameutaka Ulimwengu wa Kiislamu kutoruhusu suala la Palestina lisahaulike akisisitiza ulazima wa kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
Habari ID: 3480666    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/10

IQNA-Katika ujumbe wake kwa kongamano la "Miaka 100 wa Kuanzishwa Hauza ya Qum nchini Iran," Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Kazi muhimu zaidi ya Hauza na taasisi ya kielimu ya vyuo vikuu vya kidini, ni kufikisha ujumbe wa wazi na kuweka msingi wa ustaarabu mpya wa Kiislamu."
Habari ID: 3480651    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/07

IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, alimtembelea Ayatullah Hossein Ali Nouri Hamedani katika hospitali moja mjini Tehran.
Habari ID: 3480649    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/07

IQNA--Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei, amesema kuwa lengo la Mwenyezi Mungu katika kwa kuweka ibada ya Hija ni kuwasilisha kielelezo kamili na kinachoelekeza namna ya kuendesha maisha ya binadamu, na akaongeza: muundo na sura ya dhahiri ya ibada hii ni ya kisiasa kabisa, huku maudhui yake yakiwa ya kiroho na ya ibada, ili kuhakikisha manufaa kwa wanadamu wote.
Habari ID: 3480637    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/04

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia utakuwa na faida kwa pande mbili na unaweza kuzifanya pande mbili hizo zikamilishane.
Habari ID: 3480555    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/18

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesema mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani katika mji mkuu wa Oman, Muscat, yamefanyika vizuri katika hatua za awali, lakini ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ina shaka kubwa kuhusu upande wa pili.
Habari ID: 3480545    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/15

IQNA – Mamia ya maelfu ya wakazi wa Tehran walikusanyika katika Msikiti wa Mosalla Imam Khomeini mnamo Machi 31, 2025, kushiriki Sala ya Idul Fitr iliyoswalishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
Habari ID: 3480478    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/01

Baraza la Idi
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya kislamu, Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema kuimarika heshima ya Uislamu na kukabiliana na dhulma na uonevu wa madola makubwa vinategemea umoja na utambuzi wa Umma wa Kiislamu.
Habari ID: 3480477    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/31

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameionya Marekani kuhusu vitiso vyake dhidi ya Iran na kusema kikosi pekee cha niaba katika eneo hili (Asia Magharibi) ni utawala wa Kizayuni ambao unavamia nchi nyingine kwa niaba ya madola ya kikoloni ya dunia na ni "lazima ung'olewe."
Habari ID: 3480474    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/31

IQNA-Wananchi Waislamu wa Iran kote nchini wamejitokeza kwa mamilioni kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, kuonyesha mshikamano na Palestina, na kulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3480454    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/28

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesema maandamano ya kimataifa ya Siku ya Quds, Ijumaa hii, "kwa msaada wa  Mwenyezi Mungu, yatakuwa moja ya maandamano bora, ya kupendeza zaidi, na yenye heshima zaidi."
Habari ID: 3480449    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/28

IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameionya Marekani dhidi ya kutumia lugha ya vitisho dhidi ya Iran.
Habari ID: 3480412    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/22

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, ombi la Rais Donald Trump wa Marekani kwamba anataka kufanya mazungumzo na Iran si lolote bali ni jaribio la "kuhadaa maoni ya umma duniani" na kutaka kuonyesha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ni upande ambao hauko tayari kutoa fursa nyingine kwa diplomasia.
Habari ID: 3480365    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/13

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyid Ali Khamenei, amesema kuwa sisitizo la baadhi ya madola ya kibabe juu ya kuandaa mazungumzo na Iran hakulengi kutatua matatizo.
Habari ID: 3480330    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/09

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Ali Khamenei, leo asubuhi (Jumatano), katika Wiki ya Rasilimali Asili na Siku ya Upandaji Miti, amepanda miche mitatu ya miti.
Habari ID: 3480309    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/05