iqna

IQNA

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA) Naibu Katibu MKuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naim Qassem amesisitiza kwamba Palestina haiko peke yake kwa sababu ulimwengu wa Kiislamu unaiunga mkono.
Habari ID: 3476247    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/14

Harakati ya Hizbullah na Kombe la Dunia Qatar
TEHRAN (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem ametuma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa "Twitter" ambapo ameipongeza Morocco kwa ushindi wa timu ya kandanda ya nchi hiyo dhidi ya Uhispania hiyo jana na kufuzu kuingia robo fainali ya mechi za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar.
Habari ID: 3476211    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/12/07

Jinai za Marekani
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah amejibu matamshi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani dhidi ya Lebanon na Hizbullah na kusema: "Marekani ndio msingi wa laana na tauni, na Hizbullah ndiyo iliyoondoa shari na laana ya Marekani nchini Lebanon na kuangamiza tauni hiyo."
Habari ID: 3476074    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/12

Jinai za Saudia
TEHRAN (IQNA)- Saudi Arabia imemfunga jela miaka 15 daktari mmoja wa kike raia wa Tunisia kwa kuweka video ya maandamano ya kuiunga mkono Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon huko Tunisia.
Habari ID: 3475975    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/10/23

Harakati ya Hizbullah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa ina nguvu na uthabiti kuliko wakati wowote ule, na kwamba taifa hili litavuka salama mtihani wa sasa kutokana na hekima ya viongozi wake.
Habari ID: 3475867    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/10/02

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Septemba 16, inasadifiana na kumbukumbu ya miaka 40 ya uhalifu wa Sabra na Shatila.
Habari ID: 3475794    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/09/16

Mapambano ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya al-Umma ya Lebanon Sheikh Abdullah al-Jabri amepongeza nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mhimili wa muqawama au mapambano ya Kiislamu.
Habari ID: 3475779    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/09/13

Harakati za Muqawama
TEHRAN (IQNA)- Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS umeonana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon mjini Beirut, ukiwa ni ushahidi wa kuzidi kushikamana kambi ya muqawama katika eneo hili.
Habari ID: 3475695    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/28

Harakati ya Hizbullah
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitizia kwamba harakati hiyo daima imekuwa bega kwa bega na watu wanaodhulumiwa katika eneo la Asia Magharibi wakiwemo wa Yemen, Iraq na Afghanistan.
Habari ID: 3475666    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/23

Muqawama
TEHRAN (IQNA) - Mwanachama mwandamizi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen Mohammad Ali al-Houthi amempongeza Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayed Hassan Nasrallah kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 40 ya kuasisiwa kwa harakati hiyo ya mapambano (muqawama) ya Kiislamu ya Lebanon.
Habari ID: 3475562    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/31

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema makombora yenye usahihi mkubwa katika kulenga shabaha ya harakati hiyo ya muqawama yana uwezo wa kupiga sehemu yoyote ya utawala haramu wa Israel; baharini au ardhini.
Habari ID: 3475541    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/26

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon anasema harakati harakati hiyo ilikataa mapendekezo kadhaa ya hongo ya kifedha ya Marekani ili kusitisha mapambano yake na utawala wa Kizayuni wa Israel .
Habari ID: 3475525    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/22

Harakati ya Hizbullah
TEHRAN (IQNA) Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Lebanon haitaki vita, lakini iwapo haitapata inachostahiki, utawala wa Kizayuni hautaruhusiwa kuchimba mafuta.
Habari ID: 3475520    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/20

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, mojawapo ya matunda muhimu zaidi ya mhimili wa Muqawama au mapambano ya Kiislamu yalikuwa ni kuuzima mpango wa Marekani wa kuanzisha Mashariki ya Kati Mpya.
Habari ID: 3475500    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/14

Muqawama (Mapambano ya Kiislamu)
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon katika mji mkuu wa nchi hiyo Beirut.
Habari ID: 3475418    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/24

Uadui wa Israel
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema hatua za utawale wa Kizayuni wa Israel katika eneo la machimbo ya gesi ya Karish ni ukiukaji wa mamlaka ya Lebanon na akaonya wazi kuwa hakuna shaka yoyote kuwa Hizbullah inayo uwezo wa kijeshi na kiusalama wa kumzuia adui mzayuni asichimbe mafuta na gesi katika eneo hilo.
Habari ID: 3475357    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/10

Harakati ya Hizbullah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa misaada yake na kwamba, haikusita hata kidogo kuisaidia Lebanon.
Habari ID: 3475296    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/26

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amehutubu kwa munasaba wa kukumbuka kuuawa shahidi Sayyid Mustafa Badruddin na kusema kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina kulikuwa ni pigo kwa nchi za Kiarabu na mataifa yote ya eneo.
Habari ID: 3475271    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/20

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, amewashukuru na kuwapongeza watu wote walioshiriki katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hivi karibuni na akasema ushiriki mkubwa wa Walebanon katika uchaguzi huo na matokeo yake yamefikisha ujumbe wa uungaji mkono kwa Hizbullah au Muqawama na silaha zake.
Habari ID: 3475268    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/20

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah ameashiria uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni na kusema tatizo la waliowengi nchini Lebanon si silaha za Hizbullah au Muqawama bali ni hali ya maisha.
Habari ID: 3475230    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/10