IQNA

Mapambano dhidi ya Wazayuni

Kiongozi wa Hizbullah aionya Israel: Mauaji yoyote yatakabiliwa na jibu kali

10:55 - August 29, 2023
Habari ID: 3477514
TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah amewaonya viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwamba mauaji yoyote yatakayofanywa ndani ya ardhi ya Lebanon ya kumlenga raia wa Lebanon, Palestina au Iran au raia wa nchi nyingineyo hayatapita bila ya jibu.
Nasrallah amesema: "Hatutaruhusu katu Lebanon iwe tena uwanja wa kufanyia mauaji, na Israel inapaswa ilijue hili vizuri".
 
Amesema adui yuko kwenye mkwamo wa kihistoria, kiutambulisho na kistratijia na hana njia ya kujitoa kwenye mkwamo humo, na kabainisha kwamba: hakuna kitisho chochote kitakachoweza kuuzuia Muqawama na harakati yake, bali kitazidisha na kuimarisha msimamo na nguvu zake.
 
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Nasrallah ametaka kuwepo mshikamano wa kweli na mateka wa Kipalestina na wafungwa wa kisiasa nchini Bahrain.
 
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, tokea siku ya mwanzo hadi leo Marekani imekuwa ndiye kamanda wa vita dhidi ya Syria na balozi wa nchi hiyo amelikiri hilo.
 
Sayyid Hassan Nasrallah ameeleza kwamba magaidi wakufurishaji wanaobeba silaha ni vikaragosi tu wanaotekeleza njama na mpango wa Marekani na akaongeza kuwa: kwa kutumia kisingizio cha DAESH (ISIS), majeshi ya Marekani yamerejea tena nchini Iraq; na kwa kisingizio hichohicho yameingia Syria ili yalikalie kwa mabavu eneo la mashariki ya Mto Euphrates.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya taifa la Syria na akasema, walipobaini kuwa mpango wa kijeshi dhidi ya Syria umeshindwa na hali ya serikali ya Damascus inazidi kuimarika, wakaamua kulitwisha vikwazo taifa hilo.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria muqawama wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusema kuwa, kupamba moto muqawama katika eneo hilo na kutokuwa na uwezo wa Israel wa kukabiliana nao kumemfanya Netanyahu ajikite kwenye suala hilo kwa kudai kuwa, yanayojiri katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni mpango uliosukwa na Iran.
Nasrallah ametupilia mbali tuhuma hizo na kubainisha kuwa muqawama na mapambano katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan yanatokana na dhamira na irada ya Wapalestina wenyewe.

3484964

captcha