iqna

IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 93
TEHRAN (IQNA) – Katika kila jamii kuna watoto ambao wamefiwa na wazazi wao kwa sababu tofauti na wanahitaji uangalizi na usaidizi. Qur'ani Tukufu, katika Sura tofauti ikiwa ni pamoja na Surah Ad-Dhuha, inaweka msisitizo wa kutunza mayatima.
Habari ID: 3477254    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/08

Sura za Qur'ani Tukufu / 92
TEHRAN (IQNA) – Linapokuja suala la fedha na mali, watu wamegawanyika katika makundi mawili: wale wanaotumia fedha zao kusaidia wengine na wale wanaojilimbikizia mali bila ya kuwasaidia wengine.
Habari ID: 3477244    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/05

Sura za Qur'ani Tukufu /91
TEHRAN (IQNA) – Kuapa kwa kitu hutokea wakati suala muhimu sana litatajwa. Katika Surah Ash-Shams ya Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu anaapa mara 11 kabla ya kuashiria jambo muhimu sana.
Habari ID: 3477232    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/03

Sura za Qur'ani Tukufu /90
Wanadamu wana lengo moja kuu, nalo ni kupata furaha kamili na ya kudumu. Hili ni lengo la kawaida lakini watu huchagua njia tofauti za kulifikia.
Habari ID: 3477221    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/01

Sura za Qur'ani Tukufu /83
Katika sheria za Kiislamu na katika jamii za Kiislamu kuna kanuni maalum za shughuli za kiuchumi na adhabu kali hutolewa kwa wale wanaofanya makosa ya kiuchumi kama vile ulaghai.
Habari ID: 3477127    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/06/10

Sura za Qur'ani Tukufu / 82
Mwanadamu ana baraka nyingi maishani, ambazo zote amepewa na Mwenyezi Mungu. Lakini wakati mwingine anazichukulia kuwa za kawaida na kushindwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema alizomtunuku.
Habari ID: 3477107    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/06/06

Sura za Qur'ani Tukufu /81
TEHRAN (IQNA) – Imesisitizwa katika vitabu vingi vya Uislamu na Qur'ani Tukufu kwamba matukio fulani yatatokea duniani mwishoni mwa dunia.
Habari ID: 3477071    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/30

Sura za Qur'ani Tukufu /80
TEHRAN (IQNA) – Kuna aya nyingi ndani ya Qur’an pamoja na Hadithi kuhusu maisha ya baada ya kifo na Siku ya Kiyama, zikiwemo aya za Surah Abasa zinazosema watu wanakimbiana siku hiyo.
Habari ID: 3477058    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/28

Sura za Qur'ani Tukufu / 79
TEHRAN (IQNA) – Kuna sababu tofauti za kutomtii Mwenyezi Mungu au kutokuwa naye, ambazo humfanya mtu kujiweka mbali na malengo matukufu ya maisha.
Habari ID: 3477037    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/24

Sura za Qur'ani Tukufu / 78
TEHRAN (IQNA)-Watu wana shauku kubwa ya kutaka kujua mustakabali wao, wakati ujao unaowangoja katika siku na miaka ijayo na unaowangoja katika maisha ya baadaye.
Habari ID: 3477021    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/20

Sura za Qur’ani Tukufu /75
TEHRAN (IQNA) - Ukweli wa kushangaza ambao watu huchukulia kawaida ni kwamba alama za vidole za kila mtu ni tofauti na za wengine wote.
Habari ID: 3476969    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/07

Sura za Qur'ani Tukufu /74
TEHRAN (IQNA) - Ulimwengu huu ni mahali pa watu kujitayarisha kwa ajili ya ulimwengu mwingine unaowangoja.
Habari ID: 3476953    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/04

Sura za Qur'ani Tukufu / 73
TEHRAN (IQNA) - Usiku huwa ni maalumu kwa ajili ya kupumzika lakini amani iliyopo katika siku hizi hupelekea baadhi ya watu kutenga sehemu hiyo kwa ajili ya ibada na kutafakari. Inaelekea kwamba kuabudu wakati wa usiku wa manane huwa na fadhila zake maalumu.
Habari ID: 3476915    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/26

Sura za Qur'ani Tukufu / 71
TEHRAN (IQNA) – Hadhrat Nuh alikuwa miongoni mwa Ulul'azm Anbiya (manabii wakuu). Kulingana na riwaya, alimwomba Mwenyezi Mungu ampe wakati wa kuwaongoza watu wake na alipewa takribani miaka 1,000.
Habari ID: 3476871    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/15

Sura za Qur'ani Tukufu /70
TEHRAN (IQNA) – Adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa madhalimu na wakanushaji Mungu iko karibu na iko karibu zaidi kuliko wanavyofikiri. Bila shaka adhabu hiyo itajiri na hakuna kitu kinachoweza kusimama katika njia yake.
Habari ID: 3476853    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/12

Sura za Qur'ani Tukufu /68
TEHRAN (IQNA) – Kalamu na inachokiandika ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu. Katika Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu ameapa kwa baraka hizi ili kuashiria umuhimu wake.
Habari ID: 3476708    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/15

Sura za Qur'ani Tukufu / 67
TEHRAN (IQNA) – Uwezo usio na kikomo wa Mwenyezi Mungu umeonyeshwa katika Sura tofauti za Qur’ani Tukufu, lakini kwa namna ya pekee katika Sura Al-Mulk, inayoashiria mamlaka na adhama ya Mwenyezi katika ulimwengu wote.
Habari ID: 3476694    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/12

Sura za Qur'ani Tukufu /66
TEHRAN (IQNA)- Mwanadamu amezungukwa na dhambi nyingi zinazomweka mbali na Mwenyezi Mungu na zinazomzuia kuwa na hali ya kiroho. Hilo hupelekea mwanadamu kuchanganyikiwa na kupoteza kusudi la kweli la maisha. Njia pekee ya kutoka katika hali hii na kufikia wokovu ni kurejea kwa Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3476689    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/11

Sura za Qur'ani Tukufu /65
TEHRAN (IQNA) - Uislamu umelipa kipaumbele maalum suala la familia na kuzingatia majukumu na wajibu maalum kwa kila mwanafamilia ili waweze kuishi pamoja kwa upendo na amani.
Habari ID: 3476670    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/07

Sura za Qur'ani Tukufu /64
TEHRAN (IQNA) – Wakati mwingine sisi mara tu baada ya kufanya jambo fulani hujuta na kujaribu kufidia kile tulichokosea. Lakini itakuja siku ambayo majuto na makosa yetu hayawezi kurekebishwa au kutufaidisha.
Habari ID: 3476654    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/04