TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani hatua ya kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE au Imarati) na utawala wa Kizayuni wa Israel na kutaja hatua hiyo kuwa ni ujinga wa kistratijia ambao bila shaka utapelekea kuimarika mhimili wa muqawama na mapambano katika eneo.
Habari ID: 3473066 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/14
TEHRAN (IQNA) - Wapalestina wanaendelea kulaani vikali hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuanzisha rasmi uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473065 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/14
Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na Rais wa Ufaransa
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa ufaransa akisema kuwa Marekani daima imekuwa ikifanya jitihada za kuua mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kuwa: Ulaya haipasi kukubali kuburutwa na Marekani na kutumbukia katika mtego wake.
Habari ID: 3473063 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/13
TEHRAN (IQNA) – Polisi katika jimbo la Minnesota Marekani wanawasaka vijana wawili ambao walimpiga na kumuumiza kiongozi wa Waislamu katika eneo hilo.
Vijana hao wawili wanakisiwa kuwa na umri wa miaka 20 hivi na mmoja ni mzungu huku mwingine akiwa na asili ya Afrika.
Habari ID: 3473050 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/09
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Tiba ya vikwazo ni kuutumia ipasavyo uwezo na fursa za ndani, na si kusalimu amri mbele ya matakwa ya Marekani.
Habari ID: 3473020 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/31
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Katika matukio ya sasa ya Marekani na harakati ya kupinga ubaguzi wa rangi iliyopo, msimamo wetu thabiti ni wa kuwaunga mkono wananchi na kulaani mwenendo wa kikatili wa utawala wa ubaguzi wa rangi wa nchi hiyo."
Habari ID: 3473011 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/29
TEHRAN (IQNA) – Jeshi la Marekani linaendelea kulaaniwa vikali kwa kuhatarisha usalama wa ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa inaruka katika anga ya Syria ikielekea Lebanon.
Habari ID: 3472997 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/25
Sheikh Mohammad Yazbek
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Baraza la Shuraa la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema harakati hiyo inaweza kupambana na kuvunja njama zote za maadui kama tulivyovunja njama zao kijeshi huko nyuma kwa kujiamini na kuwa macho.
Habari ID: 3472956 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/12
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
TEHRAN (IQNA) -Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, kusema urongo na kueneza chuki ni viungo muhimu katika sera za kigeni za Marekani.
Habari ID: 3472946 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/10
TEHRAN (IQNA) – Washiriki katika maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi Marekani walisikika wakitamka Takbir yaani Allahu Akbar.
Habari ID: 3472943 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/09
Msomi wa Iran
TEHRAN (IQNA) – Msomi wa Iran Dkt. Hakimeh Saghaye-Biria, amesema taasisi za utafiti nchini Marekanizinatumiwa kupanga sera za serikali ya nchi hiyo kuhusu ulimwengu wa Kiislamuna hasa dhidi ya harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu.
Habari ID: 3472940 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/08
Zarif akihutubu katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, wizara yake inatekeleza mkakati wa kusambaratisha njama za kiuchumi za Markeani dhidi ya Iran.
Habari ID: 3472930 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/05
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema nchi za Ulaya na Marekani ni washirika wa kundi la kigaidi la Munafikin (MKO) katika mauaji ya watu wa Iran.
Habari ID: 3472909 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/29
TEHRAN (IQNA) - Hujuma ya majeshi ya kigaidi ya Marekani kwa ushirikiano na waitifaki wao Iraq dhidi ya vituo vya Brigedi za Kata'ib Hizbullah imelaaniwa vikali kote katika nchi hiyo.
Habari ID: 3472900 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/26
TEHRAN (IQNA) – Ayatullah Muhsin Araki, mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu Iran, amewatumia ujumbe wa video vijana wanaoandamana kote duniani hakitaka haki na uadilifu duniani.
Habari ID: 3472879 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/20
TEHRAN (IQNA) – Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeunga mkono kikao maalumu cha Baraza la Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa ambacho kimeitishwa kujadili ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Habari ID: 3472875 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/18
TEHRAN (IQNA)- Mashirika ya Waislamu nchini Marekani yamejiunga na wimbi la malalamiko ya kuishinikiza serikali ya nchi hiyo ifanye mageuzi haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kuondoa ubaguzi wa rangi wa kimfumo katika muundo wa polisi ya nchi hiyo.
Habari ID: 3472871 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/16
Katika maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi
TEHRAN (IQNA) - Waandamanaji wenye hasira nchini Marekani wanaendeleza mkakati wa kuanugusha, kuharibu ama kuondoa masanambu ya wabaguzi wa rangi hasa Christopher Columbus.
Habari ID: 3472858 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/12
Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) -Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema ‘kubinya shingo kwa kutumia goti’ ni sera ya daima ya Marekani na kuongeza kuwa: “Katika kipindi chote cha historia, Marekani imekuwa ikitumia sera hiyo kukandamiza madhulumu.
Habari ID: 3472854 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/10
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Harakati ya Al-Sadr ya nchini Iraq ameitaka Marekani iviondoe mara moja vikosi vyake vyote katika ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3472848 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/09