IQNA

Marekani imeua raia wasiopungua 13,000 Iraq na Syria tokea mwaka 2014

19:57 - November 20, 2020
Habari ID: 3473376
TEHRAN (IQNA) – Asasi moja ya kufuatilia mambo ya vita imesema uchunguzi wake umebaini kuwa Jeshi la Marekani limeua raia 13,000 nchini Iraq na Syria katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Taarifa ya Airwars imebaini kuwa tokea muungano wa kivita wa Marekani uliopozanisha kampeniya kile ilichodai kuwa ni magaidi wa ISIS huko Iraq na Syria mwaka 2014, idadi kubwa ya raia wameuawa.

Ushahid huo sasa utawawezesha watu wa Syria na Iraq kufuatilia fidia kutoka kwa Marekani na waitifake wake.

Kwa mujibu wa data za shirika hilo linalofuatilia madai ya kuuawa raia katika hujuma hizo hususan za anga, raia kati ya 8,310 hadi 13,187 wameuawa tokea Marekani ianzishe eti mashambulizi dhidi ya ISIS katika nchi hizo mbili za Kiarabu mwaka 2014.

Myles Caggins, aliyekuwa msemaji wa muungano huo vamizi wa eti kupambana na magaidi wa Daesh unaoongozwa na Marekani ameliambia shirika la Airwars kuwa, lengo la kuweka hadharani data hizo hivi sasa ni kuonyesha uwazi.

Hata hivyo takwimu zinazotolewa na Marekani kuhusu raia wanaouliwa huko Iraq na Syria katika mashambulizi yanayoongozwa na nchi hiyo ni ndogo mno ikilinganishwa na idadi kubwa ya raia waliouawa hadi sasa.

Jinai za muungano wa Marekani unaodai kuendesha vita dhidi ya genge la kigaidi la Daesh (ISIS) katika nchi za Iraq na Syria, dhidi ya raia wasio na hatia zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara katika nchi hizo za Kiarabu.

3473166

Kishikizo: syria ، iraq ، marekani ، isis au daesh ، raia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha