IQNA

Iraq kuishtaki Marekani kutokana ukiukwaji wa mamlaka

18:10 - December 15, 2020
Habari ID: 3473458
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Iraq imepanga kuishtaki Marekani kutokana na kitendo cha wakuu wa Washington kukiouka mamlaka ya kujitawala ya Iraq.

Mshauri ya kamati ya sera za kigeni katika Bunge la Iraq amesema wataishtaki pia Marekani kwa hatua yake ya kutumua silaha zilizopigwa marufuku katika maeneo ya raia nchini humo.

Hatif al-Rikabi amesema Iraq itawasilisha kesi hizo katika mahakama za Sweden na Ujerumani kuhusu jinai ambazo Marekani imetanda katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Amesema kila mwezi kesi mpya za saratani hurekodiwa Iraq na ushahidi unaonyesha kuwa ugonjwa huo nchini humo unasababishwa na silaha ambazo Marekani inatumia.

Vita vya Marekani Iraq vimepelekea kuachwa mabaki ya silaha zenye madini ya urani na kemikali zigine za sumu.

3473410

Kishikizo: iraq marekani silaha
captcha