iqna

IQNA

Rais Hassan Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kukaribia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kuwa, Quds (Jerusalem) katu haitasahauliwa na haitaendelea kubakia katika uvamizi wa madhalimu.
Habari ID: 3472785    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/20

Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Intifadha ya taifa la Palestina imeshavuka mipaka ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuingia kwenye awamu itakayoamua hatima yake na akasisitiza kwamba: Minong'ono ya kufikia tamati Israel ghasibu inasikika kwenye mitaa ya Tel Aviv.
Habari ID: 3472784    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/20

TEHRAN (IQNA) - Majlisi ya Ushauri ya Kiisalmu (Bunge la Iran) imeidhinisha muswada wa namna ambavyo Iran itakabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika upeo wa kitaifa na kimataifa.
Habari ID: 3472779    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/19

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Siku ya Kimataifa ya Quds itaadhimishwa nchini Iran na pia Swala ya Idul FItr itaswaliwa kwa kuzingatia kanuni za afya kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19.
Habari ID: 3472770    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/16

TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje Iran imetoa tamko kuhusu siku ya "Nakba" yaani siku ya nakama ya kuasisiwa utawala pandikizi wa Kizayuni katika ardhi walizoporwa Wapalestina na kusisitiza kuwa, kadhia ya Palestina itaendelea kuwa suala kuu nambari moja katika ulimwengu wa Kiislamu licha ya kufanyika njama nyingi za kulisahaulisha.
Habari ID: 3472767    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/15

TEHRAN (IQNA) - Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imepasisha kwa kauli moja muswada wa dharura wa kukabiliana na njama na uhasama za utawala wa Kizayuni wa Israel, dhidi ya amani na usalama wa kieneo na kimataifa.
Habari ID: 3472759    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/12

TEHRAN (IQNA) – Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu yanatazamiwa kufanyika katika ukumbi wa Instagram na mitandao mingine ya kijamii nchini Afrika Kusini, kutokana na janga la corona.
Habari ID: 3472758    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/12

TEHRAN (IQNA) - Swala ya Ijumaa imeswaliwa kusaliwa hii leo katika miji mikubwa na midogo ipatayo 157 na mikoa 21 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baada ya kusitishwa tokea mapema mwezi Machi mwaka huu kutokana na mripuko wa ugonjwa wa COVID-19 au corona.
Habari ID: 3472745    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/08

Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Japan
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Hakuna njia nyingine ya kukabiliana kwa mafanikio na corona isipokuwa kushirikiana nchi zote"
Habari ID: 3472737    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/05

TEHRAN (IQNA) - Vikao vya qiraa ya Qur'ani Tukufu vinafanyika katika hospitali na vituo vya tiba katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472734    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/04

TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema misikiti iliyokuwa imefungwa kuzuia kuenea corona (COVID-19) nchini itafunguliwa katika 'maeneo meupe', yaani maeneo ambayo hatari ya kuenea corona ni ndogo.
Habari ID: 3472732    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/04

Spika wa Bunge la Iran
THERAN (IQNA) - Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu, Bunge la Iran, amesema katika kadhia ya ugonjwa wa corona (COVID-19), ubinadamu umeporomoka na kadhia hii inatazamwa kibiashara.
Habari ID: 3472729    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/03

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuyanufaisha mataifa mengine uzoefu wake katika suala la kupambana na ugonjwa wa corona au COVID-19.
Habari ID: 3472725    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/02

TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani hatua ya chuki ya serikali ya Ujerumani ya kuiita Harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi na kusema kwamba, uamuzi huo unahudumia malengo ya utawala haramu wa Israel na Marekani.
Habari ID: 3472721    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/01

TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Utamaaduni cha Jamhuri ya Kiislamu Iran nchini Tunisia kimeandaa mafunzo ya usomaji Qur’ani Tukufu kwa njia ya intaneti katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472716    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/29

TEHRAN (IQNA)- Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiisamu ya Iran vilitoa taarifa na kuonya kwamba: Kuundwa miungano ya urongo kwa uongozi wa Marekani kwa kizingizio eti cha kusimamia usalama wa meli ni hatua ya hatari na wakati huo huo inavuruga amani na usalama wa eneo.
Habari ID: 3472712    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/28

Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na rais wa Afrika Kusini
TEHRAN (IQNA)- Marais wa Iran na Afrika Kusini wamesisitiza kuhusu kuimarishwa uhusiano wa pande mbili katika nyanja za biashara na uchumi na pia wakasema kuna udharura wa kubadlishana uzoefu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona sambamba kuboresha ushirikiano wa kiafya na kisayansi.
Habari ID: 3472711    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/28

TEHRAN (IQNA)- Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia mwanazuoni mujahidi na mwanamapinduzi marhum Ayatullah Ibrahimi Amini ambaye pia alikuwa mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.
Habari ID: 3472702    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/25

TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inafuatilia kwa karibu sana nyendo za Marekani na kuongeza kuwa: "Iran katu haiitakuwa muanzishaji wa taharuku na mapigano katika eneo."
Habari ID: 3472701    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/25

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
TEHRAN (IQNA)- Ayatullah Ibrahimi Amini mwanazuoni maarufu, mwakilishi wa watu wa Tehran katika Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu na mwanachama wa Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu Iran ameaga dunia na kurejea kwa Mola wake baada ya kuugua kwa muda.
Habari ID: 3472700    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/25