Wananchi wa Iran wameendelea kuandamana kulaani kwa nguvu zao zote ufidhuli wa jarida ya Charlie Hebdo la Ufaransa wa kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na pia kitendo cha maadui wa Uslamu cha kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Malmö wa kusini mwa Sweden.
Habari ID: 3473163 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/13
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekosoa hatua ya kuanzishwa uhusiano rasmi wa kidiplomasia kati ya Bahrain na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa, kitendo hicho ni cha fedheha na kudhalilisha.
Habari ID: 3473162 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/12
TEHRAN (IQNA) –Wajumbe wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) leo wametoa taarifa ya pamoja na kulaani vikali kujunija heshima Mtume Muhammad SAW pamoja na Qur’ani Tukufu barani Ulaya.
Habari ID: 3473161 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/12
TEHRAN (IQNA) - Wananchi wa Iran wanaendelea kufanya maandamano katika maeneo mbali mbali kupinga hatua ya kuvunjia heshima Mtume Muhammad SAW nchini Ufaransa.
Habari ID: 3473156 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/10
TEHRAN (IQNA) – Mashauriano yanaendelea kuhusu uwezekano wa kufanyika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur’ani ya Iran kwa njia ya intaneti.
Habari ID: 3473151 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/09
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelaani vikali hatua ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na kusisitiza kuwa: Njama hizo za Marekani na utawala wa Kizayuni ni dhambi isiyosameheka.
Habari ID: 3473148 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/08
Ayatullah Nouri Hamedani
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni wa ngazi za juu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu ni njama za vituo vya kifikra vya Utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani katika fremu ya kueneza chuki na hofu dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3473142 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/06
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Walimu wa Chuo Kikuu cha Kidini (Hawza) cha Qum hapa Iran imelaani vikali kuvunjiwa heshima matukufu ya Qur'ani Tukufu na Mtume Muhammad SAW na kusisitiza kuwa, kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa kisingizio cha uhuru wa itikadi kwa hakika ni kuukata roho uhuru huo na kungamiza kijinai, itakadi ya watu.
Habari ID: 3473137 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/04
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali hatua ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW).
Habari ID: 3473135 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/04
TEHRAN (IQNA) – Klipu ya sauti ya qiraa ya Qarii Mu iran i Ustadh Kabir Qalandzadeh akisoma aya za Sura Sabah ya Qur’ani Tukufu imesambazwa katika mitandao ya kijamii.
Habari ID: 3473116 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/29
Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia siku hizi za maombolezo na kukumbuka mauaji ya Imam Hussein AS, mjukuu wa Mtume Muhammad SAW na kusema: "Taifa la Iran limepata ushindi kwa kusimama kidete na kupambana na njama za madola makubwa, na ushindi huo umetokana na kufuata utamaduni wa Ashura."
Habari ID: 3473107 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/26
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, mipango ya uchumi kwa ajili ya nchi haipaswi kusimama na kusubiria kuondolewa vikwazo au matokeo ya uchaguzi wa nchi fulani na kusisitiza kwamba, uchumi wa nchi kwa namna yoyote ile haupaswi kufungamanishwa na matukio ya nje kwani hilo ni kosa la kistratejia.
Habari ID: 3473096 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/23
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, matukio yanayojiri leo hii huko Afghanistan ni matokeo ya uingiliaji na uwashaji moto wa vita uliofanywa na Marekani ndani ya nchi hiyo.
Habari ID: 3473081 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/18
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesema kuwa: kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuisaliti Qurani Tukufu na kumpa mgongo Mtume wa Mwenyezi, Muhammad SAW
Habari ID: 3473078 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/17
TEHRAN (IQNA)- Marekani imefedheheka duniani baada ya kushindwa katika jitihada zake za kulishawishi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa urefusha muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3473069 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/15
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani hatua ya kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE au Imarati) na utawala wa Kizayuni wa Israel na kutaja hatua hiyo kuwa ni ujinga wa kistratijia ambao bila shaka utapelekea kuimarika mhimili wa muqawama na mapambano katika eneo.
Habari ID: 3473066 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/14
Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na Rais wa Ufaransa
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa ufaransa akisema kuwa Marekani daima imekuwa ikifanya jitihada za kuua mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kuwa: Ulaya haipasi kukubali kuburutwa na Marekani na kutumbukia katika mtego wake.
Habari ID: 3473063 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/13
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kufuatia tukio la mlipuko katika bandari ya Beirut nchini Lebanon na kutangaza kuwa pamoja na serikali na wananchi wa nchi hiyo katika kipindi hiki kigumu.
Habari ID: 3473039 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/06
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) amesema academia hiyo inapaswa kuongoza duniani katika ustawi wa sayansi na teknolojia.
Habari ID: 3473037 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/05
TEHRAN (IQNA) – Rais Hassan Rouhani wa Iran amemtumia ujumbe wa rambi rambi mwenzake wa Lebanon Michel Aoun kufuatia miripuko iliyojiri katika mji mkuu wan chi hiyo Beirut.
Habari ID: 3473035 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/05