TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Idara ya Hija na Ziyara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea matumaini yake kuwa, janga la COVID-19 au corona litamalizika utakapowadia msimu wa joto na kwamba Hija itafanyika kama ilivyopangwa. Hatahivyo ameongeza kuwa, Iran iko tayari kwa hali yoyote itakayojitokeza kuhusu Ibada ya Hija mwaka huu.
Habari ID: 3472643 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/07
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa vyuo vya kidini katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia barua Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, na kusema vyuo vya kidini Iran viko tayari kubadilishana uzoefu na vyuo vya kidini na viongozi wa dini za mbinguni kote duniani.
Habari ID: 3472634 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/05
Brigedia Jenerali Mohammad Baqeri
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya Ulinzi vya Iran ameashiria harakati za kijeshi za Marekani nchini Iraq na katika eneo la Ghuba ya Uajemi na kueleza kuwa Marekani itakabiliwa na jibu kali iwapo itachua hatua au kutaka kuteteresha usalama wa Iran.
Habari ID: 3472626 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/02
Iran yatahadharisha
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria harakati za wanajeshi wa Marekani huko Iraq na kueleza kuwa, harakati hizo mbali na kukiuka mamlaka ya kitaifa ya Iraq zinasababisha ghasia na ukosefu wa amani katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3472625 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/02
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ameashiria vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema: Madaktari na wananchi wa Iran daima wamekuwa wakifanya mambo yanayolipa fahari taifa hili na sasa wanapata mafanikio katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19 au corona na kusimamia vyema masuala ya nchi.
Habari ID: 3472614 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/29
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mpango wa kuwachunguza watu kiafya nchini Iran kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 au kirusi cha corona ni kazi kubwa ya kujivunia.
Habari ID: 3472612 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/29
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ili kukabiliana ugonjwa wa COVID-19 au corona, ni lazima kutekelezwa kikamilifu na kwa uangalifu mpango wa 'kutokaribiana watu' (social distancing) nchini Iran.
Habari ID: 3472609 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/28
Katika Barua ya Nchi 8 kwa Katibu Mkuu wa UN
TEHRAN (IQNA)- Iran, Russia, China, Cuba, Korea Kaskazini, Iraq, Venezuela na Nicaragua zimemuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo mbali na kusisitiza kuwa ugonjwa wa COVID-19 aucorona ni adui wa pamoja wa nchi zote, zimetahadharisha kwamba, vikwazo vina taathira hasi na mbaya kwa udhibiti wa maambukizi ya ugonjwa huo.
Habari ID: 3472605 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/26
Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Iran ametangaza mipango na mikakati mipya ya kudhibiti maambukizi ya kirusi cha corona hapa nchini ndani ya wiki mbili zijazo.
Habari ID: 3472604 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/26
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani haiaminiwi hata kidogo na kuongeza kuwa: "Wakati Marekani inatuhumiwa kutegeneza kirusi cha corona, ni mwanadamu yupi mwenye akili atakubali msaada wa nchi hiyo."
Habari ID: 3472592 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/22
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS usiku wa kuamkia leo amezungumza kwa simu na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu na kulaani vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.
Habari ID: 3472591 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/22
Rais wa Iran katika ujumbe maalumu wananchi wa Marekani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe maalumu wananchi wa Marekani akitahadharisha kuwa: Siasa zozote za uono finyu na za uhasama zitazolenga kudhoofisha mfumo wa utabibu na kuviwekea mpaka vyanzo vya fedha vya kushughulikia hali mbaya iliyoko Iran zitakuwa na athari ya moja kwa moja kwa mchakato wa kupambana na janga la dunia nzima la corona katika nchi zingine.
Habari ID: 3472588 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/21
Zarif katika mhojiano na Folha de S.Paulo
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa amesema kuwa, ugaidi wa kimatibabu wa Marekani unatatiza mapambano athirifu dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo vinavyoenea kwa kasi duniani.
Habari ID: 3472587 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/21
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wa Nairuzi*
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka mpya wa Ki iran i wa 1399 Hijria Shamsia ulioanza leo nchini Iran kuwa ni Mwaka wa Ustawi Mkubwa katika Uzalishaji na kusema: Hatua kubwa ya uzalishaji inapaswa kuleta mabadiliko yanayohisika katika maisha ya wananchi.
Habari ID: 3472584 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/20
Rais Hassan Rouhani katika ujumbe wa Nairuzi*
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Iran ametuma ujumbe wa munasaba wa mwaka mpya wa Ki iran i wa 1399 Hijria Shamsiya na kusema mwaka mpya utakuwa mwaka wa afya, ajira na ustawi wa kiuchumi na kiutamaduni nchini Iran.
Habari ID: 3472583 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/20
TEHRAN (IQNA) – Idara ya Masuala ya Misikiti katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema sala za jamaa zimesitishw kwa muda katika misikiti kote nchini ikiwa ni katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona.
Habari ID: 3472581 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/19
TEHRAN (IQNA) – Mwandishi habari Mmarekani anayeishi nchini Iran amesema anafadhilisha kubakia Iran wakati huu wa kuenea maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona kutokana na ukarimu na mshikamano wa Wa iran i katika kukabiliana na uvonjwa huu.
Habari ID: 3472578 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/18
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Alhamisi usiku alitoa amri kwa Meja Jenerali Mohammad Baqeri Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutaka kamandi hiyo iunde 'Kituo cha Afya na Matibabu' kwa lengo la kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ambao ni maarufu kama kirusi cha Corona.
Habari ID: 3472561 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/13
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewasilisha orodha ya vifaa vya kitiba ambavyo Iran inahitajia kwa dharura ili kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID-19 au Corona.
Habari ID: 3472560 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/13
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameafiki pendekezo kuwa, wafanyakazi wa sekta ya afya wanaofariki wakiwa katika mstari wa mbele wa kupambana na ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama Corona wahesabiwe kuwa ni mashahidi.
Habari ID: 3472553 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/11