TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Wahadhiri katika Chuo cha Kiislamu cha Qum, nchini Iran imelaani vikali pendekezo la serikali ya Ufaransa la kuweka vizingiti katika harakati za Kiislamu nchini humo.
Habari ID: 3473250 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/11
Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani haitaweza kuvunja mapambano na muqawama wa taifa la Iran kwa kuweka vizingiti vya kununua na kudhamini dawa na chakula.
Habari ID: 3473244 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/09
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa na kusema jina za utawala wa Kizayuni wa Israel zimechupa mipaka.
Habari ID: 3473219 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/01
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje ya Iran amejibu madai ya uongo yaliyotolewa na Saudi Arabia ikisema kuwa imenasa kundi la magaidi lenye mfungamano na Iran na kusema: Watawala wa Saudia wanapaswa kuchagua njia ya ukweli hekima na busara badala ya kueneza uzusha na imlaa wanazopewa na madola mengine.
Habari ID: 3473217 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/30
Kamanda Mkuu wa IRGC
TEHRAN (IQNA) - Meja Jenerali Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa, tadbiri na busara za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu zimefelisha njama na malengo ya kisiasa ya adui katika Ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3473214 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/29
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezitaka nchi za Armenia na Azerbaijan zijizuie na zisitishe mapigano yanayoshuhudiwa katika mpaka wa nchi mbili hizo tokea jana Jumapili.
Habari ID: 3473210 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/28
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Idara ya Masuala ya Qur’ani katika Shirika la Wakfu la Iran amesema mashindano ya kitaifa ya Qur’ani nchini Iran mwaka huu yatafanyika kwa njia ya intaneti.
Habari ID: 3473207 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/27
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akihutubu katika mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani amesema: "Marekani haiwezi kutulazimisha kufanya mazungumzo wala kuanzisha vita dhidi yetu" na akasisitiza kwamba, sasa ni wakati wa walimwengu kusema "la" kwa ubabe na utumiaji mabavu.
Habari ID: 3473196 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/23
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia ushindi mkubwa na wa wazi wa taifa la Iran katika Vita vya Kujitetea Kutakatifu na kusema kuwa: Kujitetea kutakatifu ni sehemu ya utambulisho wa kitaifa wa Iran.
Habari ID: 3473189 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/21
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumapili imetoa tamko rasmi na kusema kuwa, Marekani ndiye mhatarishaji mkubwa wa usalama na amani katika kona zote za dunia.
Habari ID: 3473186 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/20
Kwa mnasaba wa Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW
TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa 34 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu utafanyika Novemba 11-13 katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran.
Habari ID: 3473178 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/17
TEHRAN (IQNA) - Mkutano wa 13 wa Baraza la Kimataifa la Mwamko wa Kiislamu umefanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran kwa lengo la kujadil namna nchi kadhaa za Kiarabu zilivyowasaliti Wapalestina kwa kuanzisha uhusiano na utawala dhalimu wa Israel unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu.
Habari ID: 3473177 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/17
Rais Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Iran ameashiria pia kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bahrain na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa, watawala wa baadhi ya mataifa ya Kiarabu katika Asia Magharibi hawafungamani na malengo ya taifa madhulumu la Palestina.
Habari ID: 3473176 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/16
Wananchi wa Iran wameendelea kuandamana kulaani kwa nguvu zao zote ufidhuli wa jarida ya Charlie Hebdo la Ufaransa wa kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na pia kitendo cha maadui wa Uslamu cha kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Malmö wa kusini mwa Sweden.
Habari ID: 3473163 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/13
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekosoa hatua ya kuanzishwa uhusiano rasmi wa kidiplomasia kati ya Bahrain na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa, kitendo hicho ni cha fedheha na kudhalilisha.
Habari ID: 3473162 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/12
TEHRAN (IQNA) –Wajumbe wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) leo wametoa taarifa ya pamoja na kulaani vikali kujunija heshima Mtume Muhammad SAW pamoja na Qur’ani Tukufu barani Ulaya.
Habari ID: 3473161 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/12
TEHRAN (IQNA) - Wananchi wa Iran wanaendelea kufanya maandamano katika maeneo mbali mbali kupinga hatua ya kuvunjia heshima Mtume Muhammad SAW nchini Ufaransa.
Habari ID: 3473156 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/10
TEHRAN (IQNA) – Mashauriano yanaendelea kuhusu uwezekano wa kufanyika mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur’ani ya Iran kwa njia ya intaneti.
Habari ID: 3473151 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/09
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelaani vikali hatua ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na kusisitiza kuwa: Njama hizo za Marekani na utawala wa Kizayuni ni dhambi isiyosameheka.
Habari ID: 3473148 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/08
Ayatullah Nouri Hamedani
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni wa ngazi za juu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu ni njama za vituo vya kifikra vya Utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani katika fremu ya kueneza chuki na hofu dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3473142 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/06