iqna

IQNA

Uuungaji mkono Palestina
IQNA (TEHRAN )- Wananchi wa Iran jana Jumanne walifanya maandamano katika mji mkuu Tehran kulaani jinai za utawala wa Kizayuni za kuwaua shahidi wanawake na watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3475605    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/10

Kiongozi wa Ansarullah Yemen
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, Sayyid Abdulmalik Badruddin Al-Houthi amesema, Imam Hussein (AS) alisimama kupambana kwa ajili ya kuuokoa Uislamu na shari ya maadui.
Habari ID: 3475598    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/09

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) – Idadi kubwa ya walowezi wa Kizayuni wenye itikadi kali waliuvamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) mapema Jumapili wakati utawala dhalimu wa Israel uikuwa ukiwashaambulia na kuwaua Wapalestina kwa mabomu huko Gaza kwa siku ya tatu mfululizo.
Habari ID: 3475592    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/07

Ukatili wa Israel
TEHRAN (IQNA)-Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imevurumisha makombora zaidi ya 100 katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina la Israel ikiwa ni katika kulipiza kisasi hatua ya utawala katili wa Israel ya kumuua kamanda wa ngazi za juu wa harakati hiyo.
Habari ID: 3475586    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/06

Rais wa Iran katika mkutano na mkuu wa Jihadul-Islami
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi amesema, leo wananchi wa mataifa ya Kiislamu ya eneo wanauchukia mno utawala ghasibu wa Kizayuni na wanaamini kuwa Muqawama na au mapambano ya Kiislamu ndio njia kuu na ya msingi ya kukabiliana na utawala huo.
Habari ID: 3475582    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/08/05

Walowezi wa Kizayuni
TEHRAN (IQNA) – Mtoto wa Kipalestina alifariki dunia masaa mawili baada ya kupigwa risasi na walowezi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliokuwa na silaha siku ya Ijumaa karibu na kijiji cha Al-Mughayer, karibu na Ramallah katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3475558    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/30

Ubaguzi wa Israel
TEHRAN (IQNA)- Afrika Kusini imeelezea wasiwasi wake juu ya ukatili unaoendelea wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina na kwa msingi huo imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuitambua Israel kama taifa la apathaidi au ubaguzi wa rangi.
Habari ID: 3475554    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/29

Kususia utawala wa Kizayuni wa Israel
TEHRAN (IQNA)- Wapalestina wamempongeza mmoja wa wanamichezo shujaa wa Algeria ambaye amekataa kwenda kucheza mpira katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel ikiwa ni kuendeleza harakati ya kimataifa ya kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestinaa na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3475552    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/29

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema makombora yenye usahihi mkubwa katika kulenga shabaha ya harakati hiyo ya muqawama yana uwezo wa kupiga sehemu yoyote ya utawala haramu wa Israel; baharini au ardhini.
Habari ID: 3475541    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/26

Njama za Israel
TEHRAN (IQNA)- Mfalme wa Bahrain amemfuta waziri mwanamke wa nchi hiyo kwa kukataa kumpa mkono balozi wa utawala haramu wa Israel mjini Manama na kwa kupinga hatua ya kuanzisha ya uhusiano wa kawaida na utawala huo haramu.
Habari ID: 3475534    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/24

Njama za Wazayuni
TEHRAN (IQNA)- Chama cha wasomi wa Kiislamu Yemen kimesema watawala wa Saudi Arabia hawastahili kusimamia maeneo matakatifu zaidi ya Kiislamu ya Makka na Madina baada Yahudi Mu israel i kuachwa kuingia katika maeneo hayo.
Habari ID: 3475528    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/23

Ubaguzi wa rangi Israel
TEHRAN (IQNA)- Wabunge katika Bunge la Kitaifa la Ufaransa wametia saini rasimu ya azimio la kulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na sera zake za ubaguzi wa rangi au apatahidi na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina.
Habari ID: 3475527    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/23

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon anasema harakati harakati hiyo ilikataa mapendekezo kadhaa ya hongo ya kifedha ya Marekani ili kusitisha mapambano yake na utawala wa Kizayuni wa Israel .
Habari ID: 3475525    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/22

Njama za Wazayuni
TEHRAN (IQNA) –Saudi Arabia inasema imemkamata raia wake ya ambaye alimuwezesha mwandishi habari Yahudi Mu israel i kuingia katika mji mtakatifu wa Makka, jambo ambalo ni kinyume cha sheria kwani wasio Waislamu hawaruhusiwi kuingia katika eneo hilo takatifu.
Habari ID: 3475522    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/22

Harakati ya Hizbullah
TEHRAN (IQNA) Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Lebanon haitaki vita, lakini iwapo haitapata inachostahiki, utawala wa Kizayuni hautaruhusiwa kuchimba mafuta.
Habari ID: 3475520    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/20

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Mamia ya Wapalestina wamefanya maandamano katika eneo la kaskazini la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupaza sauti zao za kupinga ziara ya Rais Joe Biden wa Marekani katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina la Israe katika safari yake ya kwanza ya Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) kama rais wa Marekani.
Habari ID: 3475504    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/15

Uzayuni na Marekani
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeitaja safari ya Rais Joe Biden wa Marekanii katika eneo la Asia Magharibi (Mashariaki ya Kati) kuwa ni kielelezo cha kivitendo cha uungaji mkono kamili wa Washington kwa Tel Aviv na imeonya kuhusu hatari ya safari hiyo kwa eneo hilo na mapambano ya Palestina.
Habari ID: 3475502    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/14

Njama za Wazayuni
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa Lebanon na katibu mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama au Mapambano ya Kiislamu amelaani vikali ufalme wa Saudia kwa kumteua mhubiri anayeunga mkono utawala haramu wa Israel kuongoza Sala wakati wa Siku ya Arafah wakati wa Hija.
Habari ID: 3475494    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/12

Uchambuzi wa kisiasa
TEHRAN (IQNA)- Mbali na kukosolewa sana safari yenye malengo ya kibeberu ya Rais Joe Biden wa Marekani huko Saudi Arabia na vilevile katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia na kuitwa Israel, lakini kile kinachodhihirika zaidi katika ukosoaji huo ni kuwa kufanyika safari hiyo sambaba na siku za kutekelezwa ibada tukufu ya Hija ni jambo ambalo haliwezi kuwa limefanyika hivi hivi bali limepangwa kufikia malengo maalumu.
Habari ID: 3475490    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/11

Sala ya Ijumaa
TEHRAN (IQNA) – Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqswa huko al-Quds (Jerusalem) ilihudhuriwa na makumi ya maelfu ya waumini Wapalestina jana, ambayo iliadhimisha Siku ya Arafah.
Habari ID: 3475480    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/09