iqna

IQNA

Uchambuzi wa kisiasa
TEHRAN (IQNA) - Kwa mujibu wa mtaalamu kutoka Ujerumani, mazungumzo kuhusu bei ya nishati na vile vile kutetea uhusiano wa kawaida kati ya Saudi Arabia na utawala wa Israel ni kati ya ajenda ya ziara ya kwanza ya Rais wa Marekani Joe Biden katika eneo la (Asia Magharibi) Mashariki ya Kati.
Habari ID: 3475468    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/06

Ibada ya Hija na kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA) - Kongamano kuhusu kadhia ya Palestina na wajibu wa Umma wa Kiislamu kuhusu Palestina lilifanyika katika mji mtakatifu wa Makka.
Habari ID: 3475463    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/05

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Kamati ya Kanisa la Presbyterian nchini Marekani imepitisha azimio la kutangaza Israeli utawala wa ubaguzi au apathaidi.
Habari ID: 3475457    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/03

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu wa Palestina Hamas imepongeza ripoti ya Ofisi ya Masuala ya Haki za Binadamu (UNOCHA) ambayo ilionyesha kuhusu madhara ya mzingiro wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza..
Habari ID: 3475456    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/03

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala katili wa Israel wamempiga risasi na kumuua kijana wa Kipalestina walipokuwa wakivamia sehemu ya kaskazini ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huku hali ya wasiwasi ikiongezeka katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na utawala huo katika wiki za hivi karibuni.
Habari ID: 3475443    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/29

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Mataifa umesema uchunguzi umebaini kuwa , Shireen Abu Akleh, mwandishihabari Mpalestina wa televisheni ya al-Jazeera ya Qatar aliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3475420    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/24

Uadui wa utawala wa Israel
TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) au UAE) kwamba kuwepo utawala pandikizi wa Kizayuni katika eneo hili ndiyo sababu ya ukosefu wa utulivu na amani kama ambavyo ndio ulioleta vitendo vya kigaidi na uharibifu katika eneo hili zima.
Habari ID: 3475399    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/20

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Jumamosi, Juni 11, 2022 huko Manchester, NH, jimboni New Hampshire Marekani, Kongamano la New England la Makanisa ya Methodist ilipitisha kwa wingi azimio lenye kichwa “Kutambua na Kupinga Ubaguzi wa Rangi Katika Ardhi Takatifu.”
Habari ID: 3475392    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/18

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Jeshi katili la utawala haramu wa Israel limewaua shahidi vijana watatu wa Kipalestina katika mji wa Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3475386    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/17

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Timu ya ngazi ya juu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema hatua ya utawala haramu wa Israel ya kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina na kuwafanyia Wapalestina vitendo vya kibaguzi ndio sababu kuu ya kushuhudiwa mawimbi ya ghasia zisizokwisha katika ardhi hizo zilizoghusubiwa.
Habari ID: 3475354    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/06/09

Mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel
TEHRAN (IQNA)- Alkhamisi tarehe 26 Mei, 2022, Bunge la Iraq lilipasisha kwa kauli moja sheria ya kutambua kuwa ni uhalifu, hatua yoyote ya kuweka uhusiano wa kawaida baina ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3475306    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/28

Jinai za kivita za Israel
TEHRAN (IQNA)- Mashirika kadhaa ya kutetea haki za Wapalestina yameikabidhi Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) maelezo ya kina kuhusu jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu zilizofanywa na utawala wa Israel wakati wa hujuma zake za kijeshi dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza mwaka 2021.
Habari ID: 3475294    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/25

Njama za Wazayuni dhidi ya al Quds
TEHRAN (IQNA) - Taasisi kadhaa za Kiislamu mjini al-Quds (Jerusalem) zimeonya dhidi ya kuzuka kwa vita vya kidini kama uamuzi wa mahakama ya Israel ambao unaruhusu Wayahudi kufanya ibada ndani ya eneo la Msikiti wa Al-Aqsa.
Habari ID: 3475289    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/24

TEHRAN (IQNA) - Spika wa Bunge la Misri ameulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kutekeleza "njama mbovu" za kuangamiza utambulisho wa Kiarabu na Kiislamu wa mji wa Quds (Jerusalem) na kuvuruga maeneo yake matakatifu ya kidini.
Habari ID: 3475281    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/22

Ansarullah
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameashiria mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida baina ya utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu na kusema mapatano kama hayo yatatoa mwanya kwa utawala wa Tel Aviv kujipenyeza zaidi Asia Magharibi.
Habari ID: 3475269    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/20

TEHRAN (IQNA)- Miaka 74 iliyopita, utawala bandia wa Israel ulitangaza uwepo wake baada ya kufanya mauaji makubwa ya umati dhidi ya Wapalestina. Siku hii inajulikana kama Siku ya Nakba.
Habari ID: 3475260    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/16

TEHRAN (IQNA)- Ushahidi wote unaonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umemuua kwa makusudi mwandishi wa habari wa kike na Mkristo wa televisheni ya Al-Jazeera ya Qatar Shireen Abu Akleh kwa mujibu mpango maalumu uliokuwe umeratibiwa tangu hapo awali.
Habari ID: 3475254    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/15

TEHRAN (IQNA)- Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limetenda jinai nyingine kwa kuushambulia kinyama mkusanyiko wa kuusindikiza mwili wa shahidi Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa kanali ya Televisheni ya al-Jazeera ya Qatar.
Habari ID: 3475248    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/14

TEHRAN (IQNA)- Mamlaka ya Ndani ya Palestina imesema inaunga mkono kuhusishwa taasisi za kimataifa katika uchunguzi kuhusu kitendo cha jinai cha askari wa Israel cha kumuua shahidi mwandishi habari Mpalestina wa Kanali ya Al Jazeera Shireen Abu Akleh.
Habari ID: 3475247    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/14

TEHRAN (IQNA)- Mashirika na makundi 250 ya kutetea haki za binadamu yametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kisheria utawala haramu wa Israel kwa jinai uliyotenda ya kumuua mwandishi habari wa Televisheni ya al-Jazeera Shireen Abu Aqleh.
Habari ID: 3475245    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/13