IQNA

Upinzani dhidi ya Israel

Mufti Mkuu wa Oman aafiki sheria ya kupigwa marufuku uhusiano na utawala haramu wa Israel

12:54 - January 01, 2023
Habari ID: 3476339
TEHRAN (IQNA)- Mufti Mkuu wa Oman ametangaza kuafiki na kuunga mkono mpango wa bunge la nchi hiyo wa kususiwa utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila uchao huko Palestina.

Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili amesisitiza kuwa: Tunaunga mkono muswada wa marekebisho ya kifungu cha 10 cha sheria ya kuharamisha na kupiga marufuku kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel ili upasishwe rasmi.

Mufti wa Oman ameongeza kuwa: Tunaunga mkono mpango huo kutokana na kuendelea hujuma, na uvamizi wa utawala ghasibu wa Israel na kukanyagwa haki za wananchi madhulumu wa Palestina.

Majuzi Baraza la Ushauri la Oman liliikabidhi Kamati wa Kutunga Sheria na Kulinda Haki ya nchi hiyo, muswada wa marekebisho ya kifungu cha 10 cha sheria ya kuharamisha na kupiga marufuku kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel ili upasishwe rasmi. Hatua hiyo ya Bunge la Oman, ni katika kukamilisha Dikrii ya Kifalme nambari 9/72 ya Oman kuhusu kuususia utawala wa Kizayuni na ambayo ilitolewa na Sultan Qaboos.

Dikrii hiyo ya Kifalme inatilia mkazo marufuku ya kuweka mikataba ya aina yoyote ile ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja baina ya taasisi na watu wa Oman na utawala wa Kizayuni wa Israel. Dikrii hiyo imepiga marufuku pia miamala na ushirikiano na mashirika yote ambayo yana manufaa au matawi yao katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel. 

4110983

captcha