IQNA

Wito wa kuanzishwa 'Umoja wa Mataifa ya Kiislamu'

9:23 - December 07, 2014
Habari ID: 2615835
Kiongozi wa Jumuiya ya Jamaatud Dawa nchini Pakistna Hafidh Saeed Ahmad ametoa wito wa kuanzishwa 'Umoja wa Mataifa ya Kiislamu' ili kutatua matatizo waliyonayo Waislamu duniani.

Ameelezea azma yake ya kumaliza 'utumwa wa nchi za Magharibi' katika hotuba aliyoitoa siku ya Ijumaa katika kongamano la siku mbili lililofanyika katika uwana wa Minar-e-Pakistan.
Hafidh Saeed ametoa wito kwa Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Shareef kutangaza mkakati wake kwa ajili ya Ummah wa Kiislamu hasa kusisitiza ushirikiano wa kiuchumi na kiulinzi baina ya nchi za Waislamu.
Kiongozi huyo wa Pakistan ametoa wito wa Jihadi ya Kimataifa kwa ajili ya kuondoa matatizo yaliyo katika Ummah wa Waislamu. Katika hotuba ya Sala ya Ijumaa, Hafidh Saeed amelaani vikali ugaidi na kusema Wapakistani hawatakubali nchi yao igeuzwe kuwa eneo la ugaidi na hujuma za kujiripua kwa mabomu.
Amesema jumuiya yake inakusudia kumaliza 'siasa za ghasia' kwa kuhubiri dini na kutoa huduma za kibinaadamu. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika chini ya anuani ya 'Nadharia ya Mataifa Mawili' na kuhudhuria na maelfu ya watu chini ya ulinzi mkali.Ameelezea azma yake ya kumaliza 'utumwa wa nchi za Magharibi' katika hotuba aliyoitoa siku ya Ijumaa katika kongamano la siku mbili lililofanyika katika uwana wa Minar-e-Pakistan.
Hafidh Saeed ametoa wito kwa Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Shareef kutangaza mkakati wake kwa ajili ya Ummah wa Kiislamu hasa kusisitiza ushirikiano wa kiuchumi na kiulinzi baina ya nchi za Waislamu.
Kiongozi huyo wa Pakistan ametoa wito wa Jihadi ya Kimataifa kwa ajili ya kuondoa matatizo yaliyo katika Ummah wa Waislamu. Katika hotuba ya Sala ya Ijumaa, Hafidh Saeed amelaani vikali ugaidi na kusema Wapakistani hawatakubali nchi yao igeuzwe kuwa eneo la ugaidi na hujuma za kujiripua kwa mabomu.
Amesema jumuiya yake inakusudia kumaliza 'siasa za ghasia' kwa kuhubiri dini na kutoa huduma za kibinaadamu. Kongamano hilo la siku mbili lilifanyika chini ya anuani ya 'Nadharia ya Mataifa Mawili' na kuhudhuria na maelfu ya watu chini ya ulinzi mkali.../mh

2615419

captcha