IQNA

Tovuti maalumu kuhusu Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Vijana wa Magharibi

4:53 - February 22, 2015
Habari ID: 2880257
Tovuti maalumu imeundwa kwa ajili ya kusambaza barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini.

Tovuti hiyo ambayo imetayarishwa na Idara ya Wanachuo wa Zamani wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa (SAW) inajumuisha barua hiyo  kamili kwa lugha mbali mbali. Kati ya lugha ya Kiafrika katika tovuti hiyo ni pamoja na Kiswahili, Kihausa, Kifulani na Kiamhari. Tovuti hiyo pia ina aplikesheni maalumu za simu za mkononi ambapo watumizi wanaweza kuusoma ujumbe huo pamoja au kusikiliza ujumbe huo kwa sauti mbali na kuwa na uwezo wa kutuma maoni yao moja kwa moja. Hii hapa link ya ukurasa huo.
Kufuatia matukio ya hivi karibuni nchini Ufaransa na mengine mfano wa hayo katika baadhi ya nchi za Magharibi ikiwa ni mwendelezo wa wimbi la kuuogopesha Uislamu katika ulimwengu wa Magharibi, Jumatano tarehe 21 Januari Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei alitoa ujumbe muhimu akiwahutubu vijana wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini na kuwataka wafanye uchunguzi kuhusiana na ukweli na taswira wanayopewa kuhusu Uislamu. Katika sehemu ya ujumbe wake huo, Kiongozi Muadhamu aliashiria mlolongo wa matukio ya miongo miwili iliyopita na kubainisha kwamba, katika miaka hii kumefanyika njama nyingi za kuionyesha dini tukufu ya Kiislamu kwamba ni ya kuogofya. Kupandikiza hisia za chuki juu ya Uislamu na kustafidi na hilo, ni jambo lenye historia kongwe katika historia ya kisiasa ya Magharibi. Kwa kuzingatia nukta hiyo ya kihistoria, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria katika ujumbe wake huo kwamba, kurasa nyeusi katika historia ya utendaji ya Ulaya na Marekani likiwemo suala la kuwafanya watu watumwa limekuwa jambo la kufedhehesha kwa Magharibi.../mh

2875774

captcha