IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Iran haibabaishwi na vikwazo au nguvu za kijeshi

6:49 - March 22, 2015
Habari ID: 3021914
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kuondolewa vikwazo ni sehemu ya mazungumzo ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo Jumamosi mbele ya hadhara kubwa ya wafanyaziara na majirani wa haram tukufu ya Imam Ali bin Mussa al-Ridha (as) mjini Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran ambapo sambamba na kuashiria mazungumzo ya nyuklia ya Iran na nchi za Ulaya na Marekani amebainisha kuwa, upande wa pili unaofanya mazungumzo na Iran hususan Marekani una haja na mazungumzo na kwamba, hitilafu zilizoko baina ya Wamarekani hazina maana kwamba, Washington haina haja na mazungumzo haya. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, salamu za Rais Barack Obama wa Marekani kwa mnasaba wa sikukuu ya Nouruz hazikuwa na ukweli na kubainisha kwamba, Marekani ndiyo sababu kuu ya mashinikizo dhidi ya taifa la Iran na imekuwa ikifanya kila iwezalo ili kulitwisha taifa hili ubeberu wake. Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, hakuna mtu ndani ya Iran ambaye hataki kadhia ya nyuklia ipatiwe ufumbuzi, bali kile ambacho taifa la Iran halikitaki ni utumiaji mabavu, ubeberu na utwishaji mambo wa Marekani. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, taifa la Iran halitishwi na vikwazo wala nguvu za kijeshi kwani limesimama kidete na liko imara. Amebainisha kwamba, katika mazungumzo yake na kundi la 5+1, Iran haifanyi mazungumzo kuhusiana na masuala yasiyo ya kimantiki. Aidha Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, inachotaka Iran ni utulivu na kushikwa hatamu na wananchi wenyewe wa mataifa ya Mashariki ya Kati, lakini siasa za Marekani ni kuleta vurugu na machafuko.../mh

3019887

captcha