Ban Ki moon ameelezea wasiwasi wa kushadidi hali mbaya ya kibinadamu nchini Yemen na kusisitiza kwamba, kabla ya kuanza mashambulio ya kijeshi nchini humo, nchi hiyo ilikuwa ikikabiliwa na hali mbaya ya uhaba wa chakula. Ban Ki moon amezitaka pia pande zote zinazopigana nchini humo kusimamisha mapigano na kuandaliwa mazingira ya kuanzishwa mchakato wa mazungumzo ya amani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba udiplomasia unaoungwa mkono na umoja huo, ndiyo njia pekee itakayoweza kuutatua mgogoro wa nchi hiyo na kuzuia kutokea vita vya muda mrefu katika eneo la Mashariki ya Kati. Matamshi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yanatolewa katika hali ambayo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne iliyopita lilipitisha azimio la kidhuluma la kuiwekea vikwazo vya silaha harakati ya wananchi inayoongozwa na Ansarullah nchini Yemen.../EM