Katika sherehe za ufunguzi huo, mbali na Rais Rouhani, viongozi mbalimbali wa serikali wakiwamo mawaziri, wabunge, maafisa wa kijeshi, mabalozi wa nchi za Kiislamu na wanazuoni na wataalamu wa Qur'ani na wanafunzi walihudhuria. Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Ali Muhammadi, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu na mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran ambalo limeandaa mashindano mashindano hayo ya Qur'an Tukufu, amesema kuwa, mashindano hayo yanafanyika kwa ngazi mbili kuu ambazo ni mashindano ya kisomo na kuhifadhi Qur'an kamili. Amesema kuwa, mashindano haya yanawakutanisha pamoja washiriki kutoka 120 nchi 85 duniani, ambapo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawakilishwa na Hassan Danesh katika mchuano wa usomaji, huku kwa upande wa kuhifadhi ikiwakilishwa na Sheikh Rajabi. Aidha Sheikh Ali Muhammadi amesema kuwa, kando na mashindano hayo kutafanyika kikao cha kimataifa cha uchunguzi wa Qur'ani siku ya Alkhamisi na kutawasilishwa kazi mbalimbali zilizofanyika hadi hivi sasa katika uwanja wa Qur'ani Tukufu na namna ya kuwashawishi watu wengine kukizingatia na kukifanyika kazi Kitabu hicho Kitakatifu.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameanza sambamba na mnasaba wa Mab’ath (kubaathiwa au kupewa utume Mtume Muhammad SAW). Mashindano hayo ya kila mwaka yataendelea kwa muda wa wiki moja hadi Ijumaa tarehe 22.
Wasomi (maqarii) na waliohifadhi Qur’ani kikamilifu kutoka nchi za Kiislamu na zisizo na Kiislamu watashiriki katika mashindano hayo ya wiki moja.
Pambizoni mwa mashindano hayo ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani, panafanyika pia duru ya 9 mkutano wa kimataifa wa utafiti wa Qur'ani unaowajumuisha wawakilishi wa zaidi ya nchi 10, vile vile kunafanyika duru ya 6 ya mkutano wa kimataifa wa kuwaenzi wanawake wanaojishughulisha na masuala ya Qurani. Halikadhalika kutakuwa na vikao 60 tofauti vya kujikurubisha na Qur'ani ambapo makari' kutoka nchini za Misri na Indonesia wanashiriki pamoja sambamba na warsha 50 maalumu za mafunzo ya Qur'ani Tukufu.../mh