IQNA

Maoneysho ya 23 ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran yafunguliwa

16:01 - June 25, 2015
Habari ID: 3318499
Maoneysho ya 23 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yamefunguliwa rasmi Jumatano jioni katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Utamaduni wa Muongozo wa Kiislamu Iran, maafisa waandamizi wa baraza la mji wa Tehran na wana wanaharakati katika uga wa Qur'ani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika katika Bustani ya Kujihami Kutakatifu, Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran Ahmad Jannati amesema kujikurubisha na Qur'ani kunapaswa kuwa hatua ya kuelekea katika amali bora na kutekeleza mafundisho yaliyojaa nuru ya Qur'ani Tukufu. Ameongeza kuwa Qur'ani Tukufu imeteremshwa ili kumpa mwanaadamu muongozo wa maisha sambamba na kumuondoa katika kiza na ujahili na hatimaye kumuwezesha mwandamu kufikia uokovu na kuelekea katika nuru na utakasifu.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mji wa Tehran Mahdi Chamran amesema kati ya fakhari kubwa za mji huu ni kuwa kila mwaka hufanyika maonyesho ya Qur'ani kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Ameongeza kuwa Tehran ndio mji wa kwanza wa Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu.
Maonyesho ya 23 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yamefunguliwa katika kumi la mwanzo la mwezi mtukufu wa Ramadhani mjini Tehran. Maonyesho hayo yatafanyika nyakati za usiku za mwezi wa Ramadhani hapa mjini Tehran na yatakuwa na ratiba na programu mbalimbali. Maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani yatakuwa na vitengo vya watoto na vijana, sanaa na turathi, kitengo cha vyuo vikuu, hijabu na utakasifu, elimu na malezi, maonyesho ya vitabu, wahudumu wa Qur'ani na wanawake na mazingira.Maonyesho mengine kama hayo ya Qur'ani ya Tehran yatafanyika pia katika miji 30 kote Iran katika mwezi wa Ramadhani kwa lengo la kueneza mtindo wa maisha wa Kiislamu.../mh

3318411

captcha