IQNA

Wanafunzi Waislamu Kenya walazimishwa kuingia Kanisani

20:46 - July 02, 2015
Habari ID: 3322404
Wazazi Waislamu nchini Kenya wamekosoa kitendo cha uongozi wa shule mbili cha kuwalazimisha wanafunzi wa Kiislamu kuingia makanisani kwa ibada.

Wazazi wa wanafunzi wa shule hizo ambazo moja ni shule ya msingi ya St. Joseph ya eneo la Kwale na nyingine ya sekondari Bura katika eneo la kaunti ya Taita-Taveta wamekosoa vikali uongozi wa shule hizo kwa kutozingatia itikadi za wanafunzi Waislamu, licha ya katiba ya Kenya kukataza kitendo hicho. Inaelezwa kuwa, viongozi wa shule hizo wamekuwa wakiwaamuru wanafunzi Waislamu kuingia makanisani na kushiriki ibada za Kikristo huku wakijua kuwa wao ni Waislamu. Abdulswamad Nassir, mmoja wa wabunge wa Mombasa katika bunge la Kenya sanjari na kukosoa kitendo hicho kinachokinzana na uhuru wa kuabudu, ameahidi kulifikisha suala hilo katika Wizara ya Elimu ya Kenya ili kuchukuliwa hatua za msingi katika uwanja huo. Kwa mujibu wa Abdulswamad Nassir, viongozi wa shule wamekuwa wakiwatishia wanafunzi Waislamu wanaopinga kuingia makanisani kuwa watawafelisha mitihani. Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni uongozi wa shule moja eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, uliwazuia wanafunzi wa kike kuingia shuleni hapo wakiwa wamevalia shungi vichwani.

3322065

captcha