Amnesty International limesema kwenye ripoti yake mpya kwamba, kuna njama za makusudi za kuimaliza jamii ya Waislamu magharibi mwa CAR. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kundi la magaidi wa Kikristo la Anti-Balaka limetishia kuanza mauaji mapya dhidi ya Waislamu. Kundi hilo limesema Waislamu wakiendelea kuwalengania Wakristo kujiunga na dini yao watawaua.
Shirika la Amnesty International limesema kuwa, hali ya Waislamu katika maeneo ya magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni mbaya mno. Shirika hilo limesema kuongezeka makundi ya magaidi wa Kikristo kumewafanya Waislamu kuwa wasiwasi mubwa na maisha magumu.
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 aliyelazimishwa kuacha Uislamu katika eneo la Sangha-Mbaéré ameiambia Amnesty kuwa: “Hatukuwa na budi ila kujiunga na Kanisa Katoliki. Anti-Balaka waliapa kuwa watatuua iwapo hatungefanya hivyo.” Amnesty International imesema Waislamu wanaoishi nje ya himaya ya vikosi vya Umoja wa Mataifa magharibi mwa CAR hawana uhuru wa kuabudu hadharani. Sala zimepigwa marufuku, nguo za kitamaduni za Waislamu haziruhusiwe na ukarabati wa misikiti ni marufuku.
Takribani misikiti 400 iliharibiwa kote CAR wakati wa kuanza vita dhidi ya Waislamu nchini humo mwaka 2013. Waislamu katika eneo hilo pia hawawezi kusimamisha Sala ya Ijumaa kwa kuhofia maisha yao.
Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia kwenye ghasia na machafuko ya kidini na kikabila mwaka 2013. Licha ya kupelekwa wanajeshi wa kimataifa pamoja na kuteuliwa serikali ya mpito bado juhudi hizo hazijaweza kumaliza mgogoro katika nchi hiyo. Pamoja na kuwa vikosi vya Ufaransa vilifika katika nchi hiyo ya Kiafrika lakini magaidi wa Anti-Balaka waliendeleza mauaji yao ya kimbari dhidi ya Waislamu.../mh