Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Islamic Movement , kadiri siku za Muharram zinavyozidi kupita ndivyo idadi ya wananchi wa Kaduna wanaojitokeza kwenye maombolezo ya Imam Husain AS inavyozidi kuwa kubwa.
Kiongozi wa Mashia nchini Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaki anahutubia vikao maalumu katika siku hizi 10 za Mwezi wa Muharram
Maombolezo ya mapambano ya Karbala yanafanyika katika miji na mikoa yote mengine ya Nigeria na wapenzi mbalimbali wa mjukuu mtukufu wa Mtume, Imam Husain AS, wanajumuika pamoja kuzungumzia na kukumbuka mapambano ya Karbala na dhulma waliyofanyiwa watu wa nyumba ya Bwana Mtume Muhammad SAW.