IQNA

Jinai

Watu 31 wauawa katika mashambulio dhidi ya Mashia nchini Pakistan

21:12 - September 28, 2024
Habari ID: 3479504
IQNA - Mapigano ya hivi punde katika eneo la Parachinar, jimbo la Khyber Pakhtunkhwa nchini Pakistan, yamesababisha vifo vya watu 31 na kuwaacha takriban 70 kujeruhiwa.

Mapigano hayo ya silaha yamekuwa yakiendelea kwa siku tano, kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Al-Alam.

Duru za karibu na Mashia wa Pakistani zinasema Takfiri na makundi yenye itikadi kali yametumia vibaya migogoro ya ardhi kuwalenga Waislamu wa madhehebu ya Shia huko Parachinar.

Licha ya juhudi za viongozi wa kikabila na serikali ya mkoa kupunguza mivutano, mpango wa kumaliza mapigano hayo umemalizika bila mafanikio.

Parachinar katika wilaya ya Kurram, inayojulikana kwa maeneo yake ya kitalii yenye mandhari nzuri katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, inapakana na Afghanistan.

Kuna wasiwasi kwamba ukosefu wa udhibiti wa mpaka huo umewapa nafasi Takfiri na makundi ya kigaidi kuanzisha mashambulizi na kuchochea ukosefu wa usalama.

Mashambulizi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika eneo hilo yametokea mara kwa mara kwa miaka mingi, na kuua wafuasi wengi wa Ahl-ul-Bayt (AS).

Mapigano marefu zaidi yalijiri mwaka 2007 ambapo makundi ya kitakfiri yalizingira mji huo.

Baadaye, kuanzia Januari 2012 hadi Januari 2013, mashambulizi 77 yalifanyika dhidi ya Mashia, na kuua 635 na kujeruhi mamia zaidi.

 

4238931

Habari zinazohusiana
Kishikizo: pakistan mashia
captcha