Ustadh Hafidh ambaye alikuwa pia msoma mashairi ya kidini katika televisheni ya taifa ya Misri aliaga dunia tarehe 4 Desemba baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Jumuiya ya wasoma mashairi ya kidini na qasida Misri chini ya uongozi wa Sheikh Mahmoud al Tahami imetoa tangaza la kuagha dunia Ustadh Hafidh na kutuma salamu za rambi rambi kwa maqarii na wasoma mashairi ya kidini kote Misri. Jumuiya hiyo imemuombea marehemu maghfira, rehema za Mwenyezi Mungu na Janna.
Khitma ya Ustadh Hafidh inafanyika leo tarehe 6 Januari katika Masjid Sayyida Nafisa mjini Cairo.
Marhum Ustadh Hafidh alikuwa amepangiwa kushiriki katika Mawlid ya Mtume SAW nchini Morocco lakini akatangulia mbele ya haki.
Ustadh Hafidh alizaliwa mwaka 1951 katika kijiji cha Al Qasasein mkoani Ismailiya nchini Misri. Alijifunza Qur’ani kutoka kwa Sheikh Mohammad Rashoun huku akiinukia na kulelewa katika familia ya yenye kuizingatia Qur’ani na hapoa alijifunza kusoma mashairi ya kidini.,