Kwa mujibu
wa tovuti ya hqmi.org, mashindano hay yamefanyika hivi karibuni kwa himya ya Jumuiya ya Kusomesha
Qur’ani Tukufu kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani.
Mashindano hayo yamefanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Al Noor katika eneo la Dire Dawa mashariki wa Ethiopia. Mashindano ambayo yalisimamiwa na jopo la majaji wataalamu yalikuwa na vitengo vya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu,kuhifadhi Juzuu 20, kuhifadhi Juzuu 10 na kuhifadhi Juzuu 5.
Sherehe ya kuwatunuku zawadi washindi imefanyika kwa kuhudhuriwa na Sheikh Omar Khadir Ombor mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu katika eneo la Dire Dawa, maulamaa, walimu wa Qur’ani na wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani. Wazungummzaji katika halfa hiyo wamesisitiza kuhusukushikamana na Qur’ani Tukufu na maadili mema katika jamii.
Karibu asilimia 60 ya wakaazi wa nchi hiyo ni Wakristo na asilimia 43 ni
Waislamu. Ethiopia inapakana na nchi za Somalia, Kenya, Sudan, Djibouti
na Eritrea,