Ayatullah Ahmad Khatami ameongeza kuwa Makkah na Madina ni miji muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu na Aal-Saud hawana haki hata kidogo ya kuwazuia mahujaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufika katika miji hiyo. Amesema kuwa, mahujaji wa Iran hawawezi kushiriki katika ibada hiyo chini ya anga ya kudhalilishwa au bila ya kudhaminiwa usalama wao. Ayatullah Ahmad Khatami aidha amekosoa vikali siasa za Saudia katika eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa, Aal-Saud ni watekelezaji wa siasa za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kwamba, wanaishambulia Yemen kwa lengo la kulinda maslahi ya Israel, kama ambavyo wanatenda jinai nchini Bahrain na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi yanayofanya jinai kubwa dhidi ya binaadamu katika nchi za Syria na Iraq.
Kwingineko katika hotuba yake, Ayatullah Khatami amebaini
kuwa,hatua
ya Marekani ya kutwaa dola bilioni mbili mali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,
ni wizi wa wazi na ni kinyume cha sheria. Ayatullah Ahmad Khatami ameyasema
hayo akijibu uamzi wa mahakama kuu ya Marekani wa kuzuia fedha hizo za Iran na
kusisitiza kuwa, viongozi wa Iran kamwe hawatokubali mali ya taifa lao kuporwa,
na kwamba, ni jambo lisilo na shaka kuwa, haki ya Iran itarejea nchini kutoka
mikononi mwa Marekani.