IQNA

Watoto Wayemen 10,000 wamepoteza maisha mwaka moja uliopita

19:18 - June 03, 2016
Habari ID: 3470355
Umoja wa Mataifa umesema watoto 10,000 nchini Yemen walio chini ya umri wa miaka mitano wamepoteza maisha kutokana na sababu za kivita nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Katika taarifa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stepane Dujarric amesema vifo hivyo vimesababisha na magonjwa yanayweza kuzuiwa kama vile kuhara na pneumonia.

Dujjaric amesema watoto hao wamepoteza maisha kutokana na kufungwa mamia ya vituo vya afya na kuangamia mfumo wa kiafia katika nchi hiyo.

Saudi Arabia ilianzisha mashambulizi ya kijeshi nchini Yemen tarehe 26 mwezi Machi mwaka jana, lengo likiwa ni kuisambaratisha harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani Rais mtoro na aliyejiuzulu wa Yemen, Abdu-Rabuh Mansour Hadi.

Takwimu zainaonesha kuwa katika hujuma za kinyama za Saudia dhidi ya Yemen, watu karibu 9,000 wameuawa wengi wao wakiwa ni raia hasa watoto na wanawake.

Idadi ya watoto Wayemeni waliouawa katika hujuma za Saudia ni 2,236. Aidha Saudia inadondosha mabomu katika mahospitali, misikiti, shule, viwanda, madaraja na miundombinu yote ya Yemen. Saudia pia inatumia mabomu yaliyopigwa marufuku katika hujuma zake za kuogofya dhidi ya wananchi wa Yemen.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umeuweka muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen kwenye jalada lake jeusi.

Msimamo huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kupitia ripoti maalumu, ambapo mbali na kukosoa vikali mashambulio ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Aal Saudi dhidi ya Yemen, amesema muungano huo ndio unaobeba dhima ya mauaji ya halaiki ya watoto wa Yemen.

/3459985


Kishikizo: yemen saudia vita watoto iqna
captcha