IQNA

Waislamu Athens, Ugiriki wapata nafasi ya kusalia Idi

17:20 - June 08, 2016
Habari ID: 3470370
Wizara ya Elimu na Masuala ya Kidini Ugiriki imetangaza kuwa Waislamu mjini Athens watatengewa nafasi maalumu kwa ajili ya Sala ya Idul Fitr, ambayo husaliwa baada ya kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wizara hiyo imesema Uwanja wa Michezo wa Amani na Urafiki (SEF) eneo la Neo Faliro na Uwanja wa Olimpiki (OAKA) katika eneo la Maroussi ni maeneo ambayo yatakuwa wazi kutumiwa na Waislamu katika sherehe za kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mapema mwezi Julai.

Makundi ambayo yanataka kutumia sehemu hizo yametakiwa kuwasilisha maombi kwa wasimamizi wa viwanja hivo kabla ya Juni 17.

Waislamu katika maeneo mengine ya Ugiriki wameshauriwa kuwasiliana na wakuu wa maeneo yao ili kujadli kuhusu sehemu za kusimamisha sala.

Waislamu Ugiriki kwa muda mrefu wamekuwa wakitaka ujwngwe msikiti mjini Athens ili kuweza kukidhi mahitaji ya jamii ya Waislamu wanaozidi kuongezeka.

/3460023

captcha